MWENGE WA UHURU WAINGIA HAI

mkuu wa wialya ya hai Novatus Makunga akiwa ameushikilia mwenge mara baada ya kukabidhiwa kutoka Manispaa  ya moshi mjini



kiongozi wa mwenge kitaifa,Capt Honest Ernest Mwanosa akizindua bwalo la kulia chakula wanafunzi la shule ya msingi kimashuku lililopo  wilayani hai
kiongozi wa mwenge kitaifa,Capt Honest Ernest Mwanosa, amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kushiriki kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi litakaloanza Agost 26 mwaka huu, kwa lengo la kuipa serikali uraisi wa kuleta maendeleo wa urahisi.

Mwanosa aliyasema hayo wilayani hai wakati  kukimbiza mwenge wa uhuru ambao ulizindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo wilayani humo

Aidha  amewataka wananchi kutambua kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kila mtanzania, kwa serikali kupata takwimu za watu itarahisisha zaidi kubaikna kwa mahitaji ya maendeleo.

Alisema kuwa ili kuwezesha serekali kuleta maendeleo katika nchi yetu ni muimu kila matanzania kushirika katika siku ya sensa ili aweze kuhesabiwa  .

Alibainisha kuwa sense ya makazi ambayo inafanyika Agosti 26 mwaka huu kwa nchi mzima itasaidia serekali kujua idadi ya wananchi wake ili kuweza kuwaletea maendeleo na iwapo hatuta shiriki katika zoezi hili basi serekali haiwezi kuleta maendeleo kwa watu wote na hata kama italeta  itawafikia wachache na sio wote.

Pia alisema katika kauli mbiu yao ya mwenge kwa mwaka huu wanahamasisha  ushiriki wa sensa kwa kili mwananchi ifikapo mwaka Agosti 26,ushiriki katika mchakato wa katiba mpya ,kupiga vita rushwa pamoja na kujinga na kukataa kupata maambukizi ya ugonjwa hatara wa  ukimwi.
Alisema kuwa kila mtanzani ana haki na wajibu wa kushiriki kutoa maoni katika katiba ya nchi ambayo katiba hiyo sio ya chama chochote ,wala ya dhebebu lolote bali ni la mwananchi wa Tanzania ambayo itazungumzia haki kwa pande zote  na itafuata sheria na haki ya bidamu ambayo aita hadhiri mtu yeyote.

Kwa upande mungine Mwanosa alisema kuwa katika swala la katiba chama chochote kisiingilie katiba ya nchi bali wananchi wachangie mawazo yao huku akiongezea kuwa katika kipindi hichi viongozi mbalimbali wanatakiwa kufanya kazi na kuacha na malumbamo ya sikuwa ya msingi ambayo hayawaletei wananchi maendeleo.

“sasa hivi muda wa malumbano ,matusi ,maandamano umesisha wanatakiwa wake pamoja washieikiane makundi ya vunjwe na wafanye kazi kwa makini  na  ili kuwaletea maendeleo wananchi”alisema mwandosa

Kwa upande wake  mkuu wa wilaya ya hai Novatus Makunga alisema kuwa jumla ya miradi mitano  yamaendeo umezinduliwa na mbio hizi za mwenge akizitaja kuwa ni pamoja na bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi wa shule ya msingi kimasuku,kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi wa zahanati ya shirimgungani ,kuweka jiwe la msingi pamoja na kuweka jiwe la msingi katika jongo la hospitali bomangombe.

Aliwa shihi wananchi wa wilaya ya hai kujitokeza kwa wingi kushiriki katika siku hiyo ya sensa ambayo wataesabiwa nyumba kwa nyumba huku akiwasihi kutoa ushirikiano kwa makarani.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post