BREAKING NEWS

Sunday, August 26, 2012

VIONGOZI WATAKIWA KUJIUNGA NA VYUO VINAVYOTOA ELIMU YA UTAWALA

VIONGOZI  mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujiunga na vyuo
vinavyotoa elimu ya uongozi na utawala,ili kujifunza  mbinu za
kuongoza jamii,hali itakayosaidia kuepuka kuiingiza nchi kwenye
machafuko yasiyo na tija yanayotokana na uroho wa madaraka kwa baadhi
ya watawala wasio kuwa na elimu hiyo.

Aidha   nchi nyingi zimekuwa zikikumbwa na machafuko mbalimbali
kutokana na viongozi wake kutokuwa na elimu  hiyo ambayo inamwezesha
kujua maana ya uongozi na jinsi ya kuweza kukabiliana na  majanga
mbalimbali yanapotokea.

Rai hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na Mkuu wa chuo cha Habari
maalumu kilichopo Ngaramtoni mjini Arusha, Jackson Kalusi wakati
akizungumza katika mahafali ya 3 ya wanafunzi waliohitimu  kozi ya
utawala na uongozi ngazi ya diploma kutoka nchi mbalimbali za Afrika,
ambapo wanafunzi 13  walihitimu masomo hayo na kutunukiwa cheti.

Hata hivyo alisema kuwa, wanafunzi walio wengi katika vyuo mbalimbali
wamekuwa wakisoma kwa mazoea huku  lengo lao likiwa ni  kupata vyeti
ili waonekane  kuwa wamesoma na wakifika maeneo yao ya uongozi
wamekuwa wakishindwa kuwa watendaji kutokana na kuwa hali hiyo
walijijengea toka awali.

Kalusi alisema kuwa,lengo chuo hicho ni  kuwaandaa wahitimu katika
kuwafundisha uongozi na utawala bora katika kuandaa kizazi cha watu
wanaojua maana ya uongozi na utawala  ambao watakuwa tayari kuindeleza
jamii na kuiepusha na machafuko yanayotaokana na uongozi mbovu.

Aidha alisema kuwa, iwapo wahitimu hao wataitumia vizuri elimu
waliyoipata itasaidia kuepusha ufisadi , matumizi mabaya ya
rasimilamali za nchi pamoja na kujilimbikizia mali ,ukabila ,udini na
itikadi za kisiasa hali ambayo itasaidia kudumisha amani katika nchi
yetu.

Aidha Kilusi  aliongeza kuwa ,wahitimu hao watasaidia  kwenye nchini
zenye machafuko hususani zilizopo katika nchi za Sahara ambapo
watalaamu wake hawana elimu ya uongozi na utawala hatua ambayo
wamekuwa wakisababishia nchi machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa
kujali maslahi yao binafsi .

"Nchi za afrika zimetawaliwa na rasimiliamli nyingi sana ,lakini
tatizo kubwa ni  kwa viongozi wake  kutokuwa na elimu hiyo ambapo
wamekuwa wakijikuta wakiingiza nchi kwenye machafuko makubwa, hivyo
kupitia mafunzo hayo wahitimu b hao kwa kiasi kikubwa wataweza kuleta
mabadiliko  katika nchi zao"alisema Kilusi.

Aidha chuo hicho kimeanza kutoa elimu hiyo mwaka 2009 nchini Uganda na
baadaye kiliamia jijini Arusha ambapo wanafunzi  kutoka Kenya,
Uganda,Ethiopia, Ruanda , Burundi, Congo, na Tanzania .

Naye  mgeni rasmi katika mahafali hayo , Askofu Dr. Samuel Mriithi
kutoka nchini Kenya alitoa rai kwa chuo hicho  kuhakikisha
kuwa,wanatoa elimu  ya kiroho  itakayosaidia kumjua  Mungu ili waweze
kuwa na hofu ya mungu wanapokuwa katika uongozi  na kuweza kuepuka
mabaya.

Pia  alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanaitumia elimu hiyo
kikamilifu na kwa vitendo zaidi  ili kuleta amani katika nchi zao
hususani nchi zenye machafuko kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kwa
kiasi kikubwa sana kuleta amani miongoni mwa wananchi wake kwa ujumla.

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Josephat Torner alisema kuwa,
mafunzo hayo yamewasaidia kuona mwanga na kuwa na mwanya wa kuweza
kuona  mbali kuhusu uongozi na utawala  kwani nchi nyingi zinatawaliwa
na migogoro inayotokana na watawala kutokuwa na elimu ya uongozi .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates