TAMASHA LA KITAMBI NOMA ARUSHA LANOGA TIMU YA WASHABIKI WA KITAMBI NOMA YA SIMBA NA YANGA WATOKA DROO

 nani zaidi yanga au simba wote tupo pamoja

 mduara nao ulikuwepo
 kinaitwa kiduku

 apo chachaaaaaa

 Kwaito nayo ilichezwa
 mkaka wa Dstv Kriss Mbajo akiwa anasoma gazeti naye alikuwepo katika tamasha hilo

 watoto nao walikuwepo katika tamasha la kitambi noma





 raha jipe mwenyewe bwana
 warembo nao walikuwepo

 washabiki wa simba wakiwa katika klabu ya 2i pub huku wakiwa wamebeba kitambaa cha yanga na kufurahi pamoja

Mtangazaji wa Triple A radio Hamza karelemela akiwa anabadilishana mawazo namdada wa libeneke la kaskazini katika tamasha la kitambi noma
Timu ya kitambi noma ya jijini Arusha katika kusherekea sikukuu ya idd wamecheza mchezo wa kirafiki na timu kwa kugawanya mashabiki wa timu ya simba na timu ya yanga wa klabu hiyo ambapo katika mtanange huo walitoshana nguvu na kwa sare ya goli 2-2.

katika mchezo huo ambao ulishirikisha wachezaji wa timu hizo ulikuwa wa vuta ni kuvute ambapo ulipeleka timu zote kutoka sare ya mabao hayo na mwishowe kujikuta wakigawana zawadi ya shilingi laki mbili pasu kwa pasu.

Akizungumzia mechi hiyo muhekaazina wa tamasha hili alisema kuwa mashindano na mechi hiyo ilienda vizuri na mchezo ulichezeshwa kwa usawa bila ya kupendelea.

Alibanisha kuwa pia kumepatikana washindi wengine ambao wamecheza michezo mbalimbali uku akibainisha kuwa kwa upande wa kukimbiza kuku Vanesa Silayo wa timu ya simba aliweza kuibuka mshindi na kuondoka na kuku huku kwa upande wa kuvuta kamba timu ya yanga ikiongoza na kuibuka na kitita cha shilingi laki moja na kwa upande wa mchezo wa kukimbia na mgunia Omega Mushi alishinda na kuibuka na kitita cha shilingi 50000

Libeneke lilizungumza na kapteni wa timu ya simba Ally Kibaji alisema kuwa tamasha hili limeenda vyema na wamelifurahia kwani wameweza kushiriki mashindano mengine huku akiwapongeza waandaaji wa tamasha hili.

Alisema kuwa kupitia tamasha hili wameweza kukutana na watu wengi na kufurahia pamoja na sio hivyo tu bali wamebadilishana mawazo baada ya shughuli za ujenzi wa taifa

kwa upande wa wadhamini wa tamasha hili ambao ni Kj securiti pamoja na 2i pub  iliyopo kijenge walisema kuwa wao wataendelea kudhamini matamasha mbalimbali ya klabu ya Kitambi na walidai kuwa matamasha haya yatakuwa endelevu.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post