Mkuu wa wilaya mpya ya Chemba iliyopo jimbo la Kondoa Kusini bw,Francis Isaack amewata madiwani wa halmashauri ya kondoa na watumishi kuwa mstari wa mbele kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunga tatizo la ajira kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuiwezesha halmashauri kupata mapato.
Akizungumza na Libeneke la kaskazini bw.Isaack amesema kuwa wakati umefika sasa kwa madiwani kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata ili wawaeze kuisaidia serikali katika kutatua matatizo mbalimbali ambayo yanawakabili wananchi ikiwa ni pamoja na tatizo kubwa la ajira kwa vijana.
Amesema kuwa viongozi hao wapo karibu na wananchi hivyo ni wazi wanafahamu fika kuwa ni miradi gani ambayo inaweza kuwekezwa katika maeneo yao ambayo mbali na kuisaidia halmashauri kupata mapato pia wananchi wataweza kupata ajira hasa vijana.
Aidha ameongeza kuwa serikali ina mambo mengi ya kuwafanyia wananchi hivyo ikiwa kama watendaji wa vijiji,kata na madiwani watashikamana kwa pamoja ni wazi kuwa watakuwa wameipunguzia mzigo serikali ambayo ina jukumu la kuhakikisha wananchi wanaishi maisha bora.
Vilevile bw,Isaack amesema kuwa lengo la kuwa na uongozi ni kuleta maendeleo katika kwa wananchi wanaowaongoza ikiwa ni kuwawezesha kupata maendeleo kutokana na rasilimali zinazowazunguka.
Pia ameeleza kanuni namba tano ya utumishi wa umma inasema ni lazima kuwe na viashiria vya vya kuonesha mafanikio ya kubadili maisha ya wananchi.
“ili kuonesha kuwa serikali kuu haiachiwi majukum yote ni lazima viongozi hawa kuanzia vijiji,kata, na madiwani waisaidie kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo mimi nawambieni ni lazima viashiria vionekane kwa vipi ni wanachi kupiga hatua kimaendeleo hapo tutakwenda vizuri”alisema bw,Isaack
Amemalizia kwa kusema kuwa faida itakayopatikana kutokana na swala hili ni pamoja na wananchi kupata maendeleo mbalimbali na kuweza kumudu maisha ikiwa ni pamoja na kujinufaisha wenyewe kwa wenyewe mfano kujenga shule,hospitali