BREAKING NEWS

Thursday, August 23, 2012

MAWAZIRI KUTOKA NCHI ZA AFRIKA KUHUDHURIA MKUTANO WA MAZINGIRA UTAKAO FANYIKA JIJINI ARUSHA KUANZIA SEPTEMBER 10HADI 14

 mkurugenzi wa mazingira wa nchi za Afrika Mounkaila Goumandakoye ambeye ni mratibu wa mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Afrika ambao unatarajiwa kufanyika jijini hapa mapema mwezi September akiongea na waandishi wa habari nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
 katibu mkuu wa mazingira kutoka ofisi ya Rais Sazi Salula akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo
mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo akiongelea mkutano huo mbele ya waandishi wa habari


MAWAZIRI  wa nchi za Afrika wanatarajia kuwasili jijini Arusha kwa ajili ya mkutano wa 14 wa mazingira utakaofanyika jijini hapa kuanzia september 10 hadi 14 mwaka huu 

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa mazingira katika nchi za afrika ambeye ndie mratibu wa mkutano huo Mounkaila Goumandakoye alisema kuwa mkutano huo utashirikisha  mawaziri wa nchi za Afrika ambapo  watazungumzia utunzaji wa mazingira na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoikumba nchi za afrika.

Alisema kuwa mkutano huu unashirikisha zaidi ya watu 3000 ambao wote watakuja kuzungumzia swala hilo .

Kwa upande wake katibu mkuu wa ofisi ya Rais mazingira Sazi Salula alisema kuwa mkutano huu ni wa 14 na kwa mwaka huu nchi yetu imepewa heshima pekee ya kuwa mwenyeji wa mkutano huu ambapo alibainisha kuwa waziri wa mazingira ndie ambaye atakuwa mwenyeji wa wageni hao ambapo alisema kuwa pia atakuwa mwenyekiti wa mkutano huu.

Salula alibainisha kuwa Tanzania imepewa heshima ya kipekee kwani imepangiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu kwa miaka miwili mfululizo ambapo ni mwaka huu wa 2012 pamoja na mwaka 2013.

 Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo ambaye ndie mwenyeji wa mkutano huu alisema kuwa  kwanza kabisa anampongeza Rais wa nchi hii  kwa kuifanya Arusha iwe mwenyeji wa mkutano huu kwani amebaini kuwa watu wa mkoa huu ni watulivu na hawapendi fujo.

Alisema kuwa mkutano huu utasidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa mkoa huu kwani wafanya biashara wengi wataweza kujiongezea kipato kupitia wageni ambao watakuja katika mkutano huu.

"unajua napenda kusema kuwa tutapata kipato kwani magari yetu yatafanya kazi ,vinyozi watanyoa wageni na hata wafanya biashara watapata wanunuzi"alisema mulongo

Aliwaomba wakazi wa mkoa wa Arusha na  mikoa jirani kuwakarimu wageni wetu ili wakenda kwao wakaletee sifa nzuri nchi yetu.

Mkutano huu unatarajiwa kutangulizwa na mikutanomingine midogo midogo ya maandalizi hadi pale itakapofika tarehe 10 ambapo utafunguliwa rasmi na kufanyika hadi september 14
 

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates