BREAKING NEWS

Thursday, August 23, 2012

MSIKITI MKUU WA IJUMAA WAINGIA KATIKA KASHFA NZITO

Kamati inayoongoza msikiti mkuu wa ijumaa jijini Arusha imeingia kwenye tuhuma ya kuyageuza na kubariki makaburi ya waislamu yaliyopo mkabala na barabara ya col midleton kuwa sehemu ya soko la mtumba kwani wamekuwa wakitoa hadi risiti kwa wachuuzi wa soko hilo kinyume na sheria.

Hayo yamegunduliwa na mwana libeneke la kaskazini wakati kilipofanya utafiti wake na kugundua kuwa ni wazi wanakamati hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Abdulazizi Mkindi wanachukuwa fedha kwa kuwatumia baadhi ya vijana fedha kiasi cha tsh.500 na hatujui fedha hizo zinafanyia nini na kama waislamu jijini Arusha wanatambua hilo.

Sakata hilo lililoripotiwa na gazeti la wiki la kutoka Arusha kuwa kuna soko la makaburini na kuituhumu halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushindwa kudhibiti wimbi la wamachinga hao wanaofanyabiashara kwenye eneo la makaburi tena kwenye fensi ya makaburi hayo kumbe kumekuwa na mchezo wa wajanja wakujipatia fedha bila ya jamii ya waislamu jijini hapa kujua.

 kipindi hiki kilifuatilia kwa kina na kukuta wafanyabiashara hao wakitozwa hadi risiti kwa malipo ya 500 kwa siku na vijana waliopewa kazi hiyo  katika hali isiyo ya kawaida hadi  kamari huchezwa kwenye makaburi hayo mchana kweupe na si jeshi la polisi wala viongozi wakamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya waliolikemea tatizo hilo la kikundi cha vijana wanaowatapeli wapiti njia kwa kuwachulia hadi simu na fedha.

Baadhi ya waislamu waliongea na kipindi hiki walilaani vikali makaburi hayo kugeuzwa soko na kituo cha kuchezea kamari ambayo wameielezea kuwa ndani ya quraan tukufu imekatazwa na pale wamelala hadi masheikh zetu huu sasa ni ukiukwaji wa maadili ya uislamu.

Nae mmoja wa waumini hao Aliyetambulika kwa jina Siraju jumaa alisema kuwa niabu kwa waislamu kupingana na aya za mwenyenzimungu na kuwa kitendo hicho ni kinyume na mafundisho ya bwana mtume (swa) na kuwa fedha tutaziacha hapa ulimwenguni na kuitaka kamati inayongoza msikiti na kusimamia makaburi hayo kuwaondoa haraka wafanyabiashara hao kabla ya waislamu kujichulia hatua wenye
.
“Ukiona munkari uondoshe kwa mkono wako,ulimi wako na au unyamaze kimya na hii ni imani dhaifu kuliko zote nasi waislamu tukemee kudhalilishwa huku”alisema jumaa.
 Tangia mwanzo kamati inayoongoza msikiti mkuu ndiyo ilikuwa inayasimamia makaburi hayo hivyo jambo lolote linalotokea kwenye makaburi hayo yapo kwenye usim,amizi wao hivyo kila kitu kinaratibiwa na kamati hiyo alisema muumini mmoja bw .Halipha Mshana

Alipopigiwa mwenyekiti wa kamati inayoongoza Msikiti mkuu wa ijumaa Abdul Azizi Mkindi  ambayo inasimamia pia makaburi hayo simu yake hakupokelewa na muda mwingine ilikuwa inaita tu kipindi hiki kinaendele kumtafuta mwenyekiti huyo ili aweze kijibu thuma za kamati yake .
 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates