WAUMINI WA KANISA KATOLIKI WAMZAWADIA PADRI GARI

WAUMINI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozali wa
Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wamempa
zawadi ya gari padri Gasto Sinkala ambaye amepata upadri hivi karibuni
mjini Arusha.

Akizungumza juzi na waandishi wa habari wakati wa misa ya shukrani ya

kupata upadri iliyofanyika kwenye Parokia ya Mirerani,Mwenyekiti wa
kamati ya misa hiyo,Nobert Olomi alisema gari hilo aina ya Suzuki
Escudo lina thamani ya sh11 milioni.

Olomi alisema waamini wameona wampe zawadi ya gari hilo ili

kumrahisishia usafiri padri Sinkala kwenye eneo lake la uinjilishaji
huko Loliondo na pia awakumbuke waamini wa Mirerani kwa sala kila
akilitumia gari hilo.

Akitoa shukrani kwa waamini wa kanisa hilo wakiongozwa na mapadri wa

Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Pastory Kijuu,Aloyce Kitomari,Raphael
Loratare na Theopil Mroso,Padri Sinkala alisema anamshukuru Mungu kwa
kufanikisha wito wake.

Padri Sinkala alisema japokuwa amelelewa katika mazingira na mikono ya

watu tofauti wakiwemo wazazi na ndugu zake hatimaye amefanikiwa kupata
daraja la upadri ambalo alikuwa na wito nao tangu akiwa mdogo.

“Namshukuru Mungu hata kunifikisha hapa leo ingawa wazazi wangu wapo

hai lakini hivi sasa wapo nyumbani Mbeya hawajashuhudia umati huu
uliopo leo hii lakini furaha yangu na yenu ndiyo furaha yao pia,”
alisema Padri Sinkala.

Kwa upande wake,Padri Mroso ambaye ni mlezi wa imani wa Padri Sinkala

alisema waamini wa Mirerani wameweka rekodi kwa kununulia gari ambalo
litamsaidia Padri huyo
kwenye uinjilishaji.

“Mirerani mpo juu kwani katika historia ya Jimbo Katoliki la Arusha

hakuna padri aliyepewa gari na waamini ninyi ni wa kwanza nadhani
vijana wa Mirerani miaka ijayo wakipata upadri mtawapa helkopta au
ndege,” alisema Padri Mroso

Naye,Padri Pastory Kijuu aliyekuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Mirerani

na ambaye anasoma chuo kikuu cha Nairobi alisema kila shughuli za
kichungaji atakayofanya Padri Sinkala watu wa Mirerani watabarikiwa.

Paroko mpya wa Kanisa Katoliki Mirerani,AlouKitomari alifurahishwa na

kitendo cha waamini hao kumpa gari Padri Sinkala kupewa gari ambalo
litamsaidia kufanya uinjilishaji huko Loliondo,Dikodiko na Samunge
wilayani Ngorongoro.

“Mimi nilipoanza upadri mwaka 1981 nilikuwa natumia baiskeli hivyo

nawapongeza kwa kumtunza gari Padri Sinkala japokuwa hata asingepata
hilo gari angetoa huduma ya upadri bila matatizo,” alisema Padri
Kitomari.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post