Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda (ICTR) inatarajia kuwa na vikao viwili kabla ya mwisho wa mwaka
huu kikiwemo kimoja cha kutoa hukumu, chanzo cha habari cha uhakika
kililiambia Shirika la Habari la Hirondelle Jumatatu.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, kutakuwaapo na hukumu moja katika kesi ya rufaa
ya afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Jean Baptiste Gatete, ambaye
anapinga adhabu ya kifungo cha maisha aliyopewa na mahakama ya awali
Machi 29, 2011 baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari na
kutekeketeza kizazi kama uhalifu dhidi ya binadamu.
Kutakuwapo
pia usikilizaji wa kesi ya rufaa ya mawaziri wawili wa zamani wa
Rwanda, Prosper Mugereneza na Justin Mugenzi katika mwezi huohuo.
Mawaziri hao wanapinga hukumu na adhabu ya miaka 30 waliyopewa Septemba
30, 2011 baada ya kutiwa hatiani kwa kula njama za kufanya mauaji ya
kimbari na uchochezi.
Mbele
ya Mahakama ya Rufaa zipo kesi nane zenye jumla ya watuhumiwa 18
zikisubiri kushughulikiwa na mahakama hiyo. Kesi hizo ni pamoja ile
inayojumuisha washitakiwa sita maarufu kwa jina la ‘’Butare’’ akiwemo
mwanamke pekee kuwahi kushitakiwa na ICTR ambaye pia alikuwa Waziri,
Pauline Nyiramasuhuko.
Kwa
mujibu wa mwendesha mashitaka mpaka sasa upande wa utetezi
haujawasilisha rufaa yake kutokana na matatizo ya lugha. Hukumu hiyo
yenye jumla ya kurasa 1,548 ilitolewa na mahakama ya awali Juni 24, 2012
kwa lugha ya Kiingereza wakati warufani wote wanajua lugha ya
Kifaransa.
Kesi
nyingine inawahusisha viongozi wawili wa kilichokuwa chama tawala
nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari cha MRND, ikiwa ni pamoja na
Matthieu Ngirumpatse na Edouard Karemera ambao walihukumiwa vifungo vya
maisha jela. Upande wa mashitaka umesema ni Ngirumpatse pekee mpaka sasa
ndiye aliyewakwishawasilisha rufaa yake wakati Karemera atafanya hivyo
pia kwa siku za usoni.
Kesi
nyingine iliyoko mbele ya Mahakama ya Rufaa pia inajulikana kwa jina la
Military II, yenye jumla ya maafisa wanne wa zamani wa jeshi la Rwanda.
Hao ni pamoja na majenerali wawili, Augustin Bizimungu na Augustin
Ndindiliyimana, Meja Francois-Xavier Nzowonemeye na Kapteni Innocent
Sagahutu.Wanapinga hukumu iliyotolewa Mei 17, 2011.
Bizimungu
alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela wakati Ndindiliyimana alihukumiwa
adhabu ya muda aliokwishatumikia tangu atiwe mbaroni Januari 29, 2000.
Nao Nzuwonemeye na Sagahatu walihukumiwa vifungo vya miaka 20 jela kila
mmoja.Pande zote mbili za mwendesha mashitaka na utetezi zimekata rufaa.
Kesi
ambazo zina warufani mmoja mmoja ni pamoja na za Meya wa zamani
Gregoire Ndahimana aliyefungwa miaka 15 jela, waziri wa zamani Calixte
Nzabonimana, aliyepewa kifungo cha maisha na afisa wa zamani wa jeshi la
Rwanda, Kapteni Idelphonse Nizeyimana ayelihukumiwa kifungo cha maisha
jela