Baadhi ya viongozi na watendaji wa CUF wakijumuika
katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, huko nyumbani
kwake Mbweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad akitoa shukrani kwa viongozi na watendaji wa CUF walioitikia
mwaliko wa futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao huko nyumbani
kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Kulia (aliyesimama) ni Mkurugenzi
wa habari na haki za binadamu wa CUF Bw. Salim Bimani