shule za kata zikiwa na uongozi thabiti na imara zinaweza kufanya vizuri kitaaluma kuliko shule za watu binanfsi.
Rai hiyoimetolewa na aliyekuwa mkuu wa shule ya Sekondari Nkoanrua iliyopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha bi.Magreth Nnko katika hafla iliyofanyika shuleni hapo kwa ajili ya kumuwaga mkuu huyo ambaye alikuwa amefikisha mda wake wa kazi na kustaafu.
Bi.Nnko amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakibeza shule za kata kutokana na akutofanya vizuri kitaaluma hivyo amewataka kutambua kuwa shule hizo zinaweza kufanya vizuri endapo kama kutakuwana uongozi thabiti na imara.
Aidha ameongeza kuwa njia muafaka ya shule kufanya vizuri kitaaluma ni lazima jamii husika kutoa ushirikiano wa karibu kwa walimu ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu bora sanjari na kuwa na nidhamu ili waweze kufanikiwa kitaaluma na shule iweze kupata maendeleo.
Amesema shida kubwa iliyopo hadi watoto kufanya vibaya ni pamoja na msongamano darasani hali ambayo inapelekea watoto wengi sana kufanya vibaya kitaaluma na kiwango cha elimu kudidimia.
Vilevile amewataka wakuu wa shule kuwa wabuni kwa kushirikiana na wazazi ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili zikiwa ni pamoja na kuongeza majengo ili kuondoa msongamano madarasani.