TAMASHA LA MAMBO JAMBO MJI ARUSHA LAFANA


Mtoto mtamu katika sauti ambae pia ni radio presenter wa MJ FM akimwaga mashairi tofauti tofauti kama wimbo wake mpya wa "RUDGALZ".Kaa tayari hivi karibuni nitahojiana nae ili ufahamu zaidi kipaji chake

 Kiukweli JCB anazimikiwa na mashabiki wengi A Town, nimeamini hili na naomba pia uamini hili, watu woote walikuwa katika majukwaa wameketi huku wakiangalia show za wasanii wengine kibao, lakini alipotajwa JCB niliona mvua ya watu wakishuka na kusogea alipokuwa JCB stegini.
 Mtoto wa kike TIGER EYES alichana na baada ya kuchana aliamua kumuachia jamaa mic na kuzungusha nyonga zake kwa ufasaha kabisa, kitu kilichowavutia mashabiki wengi huku wakisikika wakisema "mmh hapo sawa!!!!"

Sikufahamu kama mtu mzima "Stopa Rhyme" yupo pande hizi, lakini alipotinga stejini shangwe zilisikika huku yeye mwenyewe akiwauliza mashabiki wake "tuanze na zipi rhymes za zamani au za sasa?
Miriam Candle ni msanii mwenyekipaji cha kuimba lakini ukiachilia mbali wimbo wake wa "mapenzi ya sasa" na ule aliofanyia video wa "Candle light", leo nimemshuhudia akichana kama hip hop vile.Poa nitamtafuta tuchonge halafu utafahamu mengi zaidi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post