Ninaomba
WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye
shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina
uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa
kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa
wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.
Shule hii
utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha
shule,yaani wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na
kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa
mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani cha
fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato
na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo
picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali
familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi
ni pale mfanyakazi anapoachishwakazi na shule kuendelea kutumia picha za
wafanyakazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa na wala
fedha hizo kuwafaidisha wenye picha nawao kutojali kuwa kitendo hicho ni
kinyume cha sheria.
Pia picha
hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura
za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani
na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu
mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui
na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi
zisikuwa zao na kupigwa picha hizo kuzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa ya
mwafunzi, wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.
Kama hiyo
aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za
msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi
mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu
na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa
kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa
haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini
mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na
umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya
wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida
inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu
Tanzania?
Linalosikitisha
zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya
kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha
wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na
kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na
wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.
Hata hivyo
nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa
kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini
wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa
ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo cha
shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza
waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia viongozi wazalendo
kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharau na kupuuza
sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo
kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za
nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa,
maslahi ya kiwango cha utumikishwaji,niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea
kiswahili na wanafunzi.