BREAKING NEWS

Thursday, August 30, 2012

FOMU ZA UCHAGUZI ARFA ZAANZA KUTOLEWA ARUSHA


 
Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha kinatarajia kufanya uchaguzi wake wa viongozi mapema september saba mwaka huu .

Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa uchaguzi huo John Bayo alisema kuwa fomu zakugombea nafasi mbalimbali zimeshatolewa na zipo tayari na mtu yeyote ambaye ni mkazi wa mkoa huu na anavigezo vya kugombea nafasi mbalimbali ajitokeze


Alisema kuwa nafasi zinazogombewa ni pamoja na mwenyekiti ,makamu mwenyekiti,katibu mkuu,katibu msaidizi,mweka hazina,mjumbe mkutano mkuu TFF,mwakilishi wa vilabu TFF pamoja na wajumbe watatu wa ARFA.


Alisema kuwa una ada za kuchukuwa fumu ambazo zinatakiwa kutolewa ambapo alisema kuwa kwa upande wa mwenyekiti anatakiwa kutolewa 200000 katibu msaidizi shilingi 200000 katibu mkuu  kiasi cha shilingi 2000000,mwenyekiti msaidizi shiingi 200000,mweka hazina shilini laki moja pamoja na ajumbe wengine wote shilingi laki moja.


Alisema kuwa mahala pa kuchukulia fomu ni katika kituo cha michezo kand ya kaskazini kilichopo ndani ya uwanja wa sheikh amri abeid jijni hapa .


Alitoa wito kwa wanachi wapenda michezo kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu hizo ambazo katika watakao chukuwa fomu ndipo watakapopata kiongozi wa michezo atakae weza kutuoendeshea soka letu vyema na mkoa wa arusha ukawa na timu.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates