kamanda wa polisi mkoani Arusha
JAMBAZI sugu lililokuwa likitafutwa kwa muda mrefu mkoani hapa,aliyetambulika kwa jina la Peter Toshi mkazi wa dareaja mbili jijini ARUSHA, amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika majibishano ya kurushiana risasi wakati akijiandaa kufanya uhalifu akiwa amefuatana na mwenzake.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea agosti 29 mwaka huu majira ya saa 5 usiku katika eneo la Sinoni daraja mbili ndani ya manispaa ya Arusha.
Sabas alisema kuwa,kuuawa kwa jambazi huyo ambaye alikuwa akitafutwa muda mrefu ni baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kuhusiana na watu hao ambao ni majambazi baada ya kuwatilia mashaka.
Alisema kuwa jambazi huyo akiwa na mwenzake walikuwa wamesimama katika eneo la bar ya tanzanite iliyopo eneo la sinoni ambapo walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kwenda kufanya uhalifu .
Alisema kuwa, baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika eneo la tukio, ambapo majambazi hao walipowaona polisi ghafla walianza kuwarushia risasi ndipo polisi walianza kujibu mapigo na hatimaye kufanikiwa kuumpiga jambazi huyo ambaye alifariki dunia.
Alifafanua kuwa, katika majibizano hayo ya risasi jambazi mwingine alifanikiwa kukimbia na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi katika kumsaka aliyekimbia.
Aidha baada ya jambazi huyo,kufariki alipekuliwa na kukutwa na silaha moja aina ya Pistol aina ya Tisas ikiwa imefutwa namba zake huku ikiwa na risasi 3 tu.
Alifafanua zaidi kuwa, jambazi huyo hivi karibuni alitoka mahabusu akikabiliwa na tuhuma mbalimbali za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha na amekuwa akiendelea na uhalifu mkoani hapa na jeshi la polisi limekuwa likimsaka kwa muda mrefu sana.
Sabas alisema kuwa, jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo, na amewaomba wananchi mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa kutosha klatikakuwafichua wahalifu wote.
Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zimedai kuwa jambazi huyo akiwa na mwenzake alipanga kwenda kufanya mauaji kwa mkazi mmoja wa eneo hilo(jina limehifadhiwa) anayedaiwa kuwa ni rafiki yao baada ya kubaini kuwa amekuwa akiwasaliti kwa kutoa taarifa zao za uhalifu kwa polisi.
Mwili wa jambazi hiuyo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitaloi ya mkoa mount meru kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi hilo likiendesha msako ka jaambazi mwingine aliyefanikiwa kutoroka.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia