WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AFARIKI DUNIA


Alikuwa na umri wa miaka hamsini na saba na ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala wake ulikumbwa na utata barani afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga amesema kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.
Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua mahala pake.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post