Mkuu
wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga amewataka viongozi wote wa vyama vya siasa na
serikali katika ngazi zote wilayani humo kutoa ushirikiano katika kuhamasisha na
kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa wananchi kushirikiana na makarani wa sensa
kwa kutoa taarifa sahihi wakati wa zoezi la kuhesabu watu.
Bw
Makunga ametoa wito huo wakati anafungua mafunzo ya wasimamizi na makarani wa
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwa wilaya ya Hai inayowashirikisha
makarani hao wapatao 644
Makunga
ametoa wito wa wananchi wilayani Hai kuendeleza ushirikiano na mshikamano kama
ambavyo wamekuwa wakifanya katika masuala mengine ya kitaifa ili kuhakikisha
kuwa sensa hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Ameeleza
kuwa utaratibu umeshaandaliwa wa kufanyika zoezi la uhamasishjai katika maeneo
yote litakalofanywa na wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na maheshimiwa
madiwani pamoja na kamati nya sense ya wilaya katika juma la mwisho kabla ya
kufanyika kwa sensa
Amewataka
makarani wote waheshimu dhamana kubwa waliyopewa na serikali kwa kuwa miongoni
mwa wananchi wapatao 2,700 walioomba kufanyakazi ya sensa kwa kuhakikisha
wanatimiza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na kwa kasi lakini yenye uhakika
Makunga
ameeleza ni muhimu kutumia elimu watakayoipata katika mafunzo hao,busara na
uwezo wao wote kutambua maeneo ya kuhesabia watu,mbinu za kuuliza maswali na
kujaza madodoso katika ngazi ya kaya,kuhakiki na kutunza madodoso na namna ya
kusimamia kazi kwa lengo la kudhibiti ubora wa takwimu zinazokusanywa.
Ameeleza
kuwa baada ya mafunzo hayo kutakuwa na mitihani ya kuwapima makarani hao katika
kile walichofundishwa kwa nadharia na vitendo
Aidha
Makunga ametumia nafasi hiyo pia kufafanua madai yanayoenezwa na baadhi ya watu
wilayani humo kuwa uongozi wa serikali wilayani humo unawachukia walimu na
ndiyo maana hawakupewa hawakuteuliwa katika sensa
Makunga
ameeleza katika kundi hilo la makarani sehemu kubwa ni walimu ambao ni 340 huku
wengine wakiwa wahitimu wa kidadto cha nne,sita na vyuo vikuu na wachache ni
watumishi wa huma.
“Tungependa
kuchukuwa watu wote 2,700 walioomba lakini kwa bahati mbaya nafasi zilikuwa ni
644 hivyo katika hizo chache tumehakikisha tunachanganya makundi yote yakiwemo
ya wazoefu na wasiokuwa na uzoefu,”alifafanua.
Ametaka
propaganda mbalimbali zonazoenezwa mitaani zipuuzwe kwani hata siku moja
serikali haiwezi kuwachukia watu wake ambao inajukumu la kuwahudumia na
kuwatendea haki.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa makarani hao, Mwalimu Fadhili Simbano amemwakikishia
mkuu huyo wa wilaya kwamba kutokana na umakini mkubwa wa kuteua makarani,wilaya
hiyo itakuwa miongoni mwa wilaya nchini ambazo zitafanya zoezi hilo kwa ufanisi
mkubwa