hichi ndicho kikosi kipya cha timu ya simba kilichocheza leo jijini Arusha na timu ya Mathare na kuibamiza magoli 2-1
mchezaji wa timu ya simba Komabil Keita akiwa anatoka nje ya uwanja mara baada ya kuumia goti
Kikosi cha timu ya Mathare UNTD ya nchini Kenya
Daniel Akuffo maskini kakosa goli Viongozi wa kubwa wa timu ya simba akiwemo mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia hanspope pamoja na makamu mwenyekiti wa simba
Waamuzi waliochezesha mechi ya simba na Mathare wakiwa wanaingia uwanjani tayari kwa mechi
Daniel Akuffo maskini kakosa goli Viongozi wa kubwa wa timu ya simba akiwemo mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia hanspope pamoja na makamu mwenyekiti wa simba
Waamuzi waliochezesha mechi ya simba na Mathare wakiwa wanaingia uwanjani tayari kwa mechi
BAO la penalti dakika ya 81 lililofungwa na kiungo Kiggi Makassy, jioni hii limeipa Simba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mathare United ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na kipindi cha pili, Simba SC inayofundishwa na Mserbia, Milovan Cirkovick ilipata bao la kuongoza dakika ya 53, mfungaji mshambuliaji kutoka Ghana, Daniel Akuffo aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Amir Maftah.
Mathare walisawazisha bao hilo dakika ya 68, mfungaji Daniel Mwaura aliyeipasua ngome ya Simba SC, iliyokuwa ikiogozwa na Paschal Ochieng na Juma Nyosso.
Beki wa Mathare alimuangusha kwenye eneo la hatari, Uhuru Suleiman dakika ya 80 na ushei na refa akaamuru ipigwe penalti, iliyopachikwa kimiani kiufundi kwa guu la kushoto la Kiggi Makassy.
Simba ilicheza vizuri mechi hiyo, leo hii Haruna Moshi ‘Boban’ akirudishwa katika nafasi ya kiungo baada ya kupatikana kwa washambuliaji halisi. Alicheza kwa utulivu, akigawa vizuri mipira na hata kuwapokonya mipira viungo wa timu pinzani.
Dakika za mwishoni ilishuhudiwa Boban akipitia mpira kwa nguvu miguuni mwa mshambuliaji wa Mathare, baada ya Maftah kupitwa, kuashiria kwamba kijana amebadilika si Yule wa kukaba kwa macho.
Feliz Sunzu na Akuffo walikuwa wanapishana vizuri pale mbele na waliitia misukosuko ngome ya Mathare- zaidi ni kwamba wawili hawa wanahitaji muda zaidi wa kucheza pamoja ili kutengeneza safu kali ya ushambuliaji ya Simba SC.
Juma Kaseja na Mrisho Ngassa hawakushiriki kabisa mechi ya leo kwa sababu walikuwa wagonjwa na Keita alimpisha Nyosso baada ya kuumia.
Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; Wilbert Mweta/Hassan Waziri, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah/Paul Ngalema, Paschal Ochieng, Komabil Keita/Juma Nyosso, Salum Kinje/Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Mwinyi Kazimoto/Haruna Shamte, Haruna Moshi, Felix Sunzu, Abdallah Juma/Amri Kiemba na Daniel Akuffo/Uhuru Suleiman.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia