Viongozi wa
chama cha wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini (TASO) wametakiwa kuta tathimini ya wakulima na
wafugaji wangapi ambao wamefaidi maonysho hayo tangu kuanza kwake.
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa mkoa wa manyara Erasto Bwilo wakati w a ufunguzi rasmi
maonysho ya wakulima na wafugaji yanane
nane yanayofanyika katika viwanja vya Taso themi njiro jijini hapa
“wanacchi
wamekuwa wakijiliza juu ya faida znazopatikana kutokana na maonyesho hayo bila
kupata jibu na kubaki ikinung’funika wasijue cha kufanya “alisema mkuu huyo
Akifafanua
zaidi alisema kuwa taso wanapaswa kujiwekea mikakati katika shughuli zote
wanazofanya ili kuondoa kuauli ya sitofahamu na kuwashindanisha wakulima hao na
kuwapa zawadi.
Aidha alisema kuwa taso inapaswa kuhakikisha
inapeleka teknolojia ya kilimo na pembejeio na ufugaji vijijini ili kuweza kuleta ushindani katika
maonyesho mengine
Naye
mwenyekiti wa taso kanda ya kaskazini Arthur Kitonga alimtaka mkuu hyo wa
mkoa kuhakikisha anashirikiana nao ili
kuweza kujenga hosteli
Hata hivyo
alimkumbusha waziri aliyekuwa na dhamana wa kilimo Profesa Jumanne Maghembe
kutekeleza ahadi ya shilingi milioni 300 ya kungania kujengwa kwa hostel ndani
ya uwanja huo wa maonyesho aliyoitoa mwaka jana kwa ajili ya wakulima
Maonyesho hayo ya wakulima na wafugaji ni ya 9
tangu kuanzishwa kwake na uadhimishwa kila mwaka na kuwakutanisha wakulima na
wafugaji pamoja na wadau mbalimbali na kwa mwaka huu yanatarajiwa kufugwa na waziri
mkuu muheshimiwa mizengo pinda