BALOZI wa Tanzania nchini China, Philip Marmo,
BALOZI wa Tanzania nchini China ambaye pia alikuwa ni mbunge wa jimbo la Mbulu,Phillip Marmo amehaidi kuliendeleza kombe la mpira wa miguu maarufu kama “Marmo Cup”ambalo lilikuwa likifanyika kila mwaka jimboni humo.
Kombe hilo lilikuwa likifadhiliwa na balozi huyo wakati akiwa mbunge wa jimbo hilo miaka yote ambapo vijana mbalimbali ndani ya jimbo hilo walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia mashindano hayo lakini tangu aondolewe lilisimama.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Equitor jijini hapa,Marmo alisema kwamba tangu aondoke kwenye nafasi yake ya ubunge mwaka juzi kombe hilo halijafanyika na hivyo amerudi kuliendeleza kwa kuwa yeye ni mdau wa michezo nchini.
“Nimesikitika sana nimekwenda sioni vijana wakicheza tena mpira wameniuliza mzee vipi hatuchezi tena mpira mimi nimewaambia nimerudi tutacheza tena”alisema Marmo
Hatahivyo,kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu(bunge) alisisitiza kwamba anafikiria kufanya mashindano hayo kuwa bila kikomo kwa kuwa yalikuwa yakiwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao vya soka.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia