AFISA MUANDAMIZI BARAZA LA HABARI TANZANIA AFARIKI DUNIA

Ofisa Mwandamizi  wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Alfred Mbogora,amefariki mapema  tarehe 18/8/2012 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya kuugua ghafla.

 Taarifa zinasema siku ya jumatano aliuguwa ghafla akiwa safarini kuelekea Bagamoyo kikazi.Ambapo njiani alisema hajisikii vizuri na kupoteza nguvu.

Marehemu Alfred Mbogora aliwahi pia kufanya kazi katika taasisi ya Utafiti na Demokrasia(REDET),amewahi kuwa mwandishi wa habari wa SHIHATA,The Guardian  na  The African.

MUNGU AILAZE  ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI-AMIN

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post