WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MANYARA WAJITOSA KUCHUKUWA FOMU Z A UVCCM

WANACHAMA watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Manyara
wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani humo.

Akizungumza  na waandishi wa habari,Kaimu Katibu wa UVCCM mkoani
Manyara Raphael Sumaye aliwataja vijana hao waliojitokeza kugombea
nafasi hiyo ya Uenyekiti ni Aloyce Pasian,Kandemeda Massala na Regina
Ndege.

Aliwataja wagombea wa nafasi moja ya Ujumbe wa Baraza la UVCCM Taifa
ni Rajabu Dago,Valleria Juwali na Kombo Vitabado huku Amani
Mshamu,Lendukus Keia na Peter Nyigu wakigombea ujumbe wa halmashauri
Kuu ya CCM mkoa.

Kaimu Katibu huyo wa UVCCM mkoani Manyara aliwataja wagombea wawili
waliogombea nafasi moja ya ujumbe wa Mkutanao mkuu wa CCM mkoani humo
ni Blandina Michael na Paschalina Emmanuel.

Aliwataja wagombea wawili wa nafasi moja ya ujumbe wa Umoja wa
Wanawake (UWT) mkoani humo ni Rachel Wade na Zahra Goda na mgombea
mmoja Emialia Alfred amegombea nafasi moja ya jumuiya ya wazazi ya
mkoa huo.

“Hata hivyo,nimefarijika mno kutokana na mwitikio wa vijana wa CCM
waliojitokeza kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za UVCCM mkoani
Manyara kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,” alisema
Sumaye.

Alisema Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM mkoani humo chini ya Mwenyekiti
wake Janes Darabe ambaye hatagombea tena nafasi hiyo kutokana na umri
mkubwa imeshayapitia majina hayo na kuyapeleka ngazi husika.

“Agosti 14 Kamati ya Siasa ya mkoa chini ya Mwenyekiti wake Lucas Ole
Mukus inatarajia kupitia majina haya kabla ya kuyapeleka kwenye ngazi
ya Taifa ambao ndiyo wenye nafasi ya mwisho ya kupitisha majina haya,”
alisema Darabe.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post