mmoja wa wachezaji wa simba akiwa ameumia katika mazoezi
kocha wa simba akiwa anawapa mazoezi wachezaji wake katika uwanja wa shule ya st.Jude jijini Arusha |
Akiongea na waandishi
wa habari mwenyekiti wa klabu ya simba jijjini hapa Afrey Mkumbo alisema
kuwa mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa juma mosi majira saa kumi katika
uwanja huo.
Alisema mechi hii ya
kirafiki itakuwa ni moja ya mechi ambazo wameziweka katika ratiba zao ambapo
alisema kuwa mbali na mechi hiyo pia wanampango wa kucheza na timu ya
chaki ya jijini hapa.
Aidha alisema kuwa
walikuwa na mpango wa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya jkt oljoro lakini
wameshindwa kutokana na timu hiyo kutokuwa na wachezaji wote hali ambayo
ilisabisha kocha wa tim u ya simba kugoma kupeleka wachezaji mbulu katika mechi
hiyo ambapo alidai kuwa ni bora wakapoteza mechi hiyo ya kirafiki.
Kwa upande wake kocha
wa timu ya simba Mserbia Profesa Milovan Cirkovick
alisema kuwa mpaka sasa mazoezi yanaenda vyema na hakuna mchezai hata mmoja
ambaye ni majeruhi na aliisifia hali ya hewa na kusema kuwa kwa sasa hali ya
hewa ni mzuri na inawazezesha wachezaji kufanya mazoezi pasipo kuchoka.
Alibainisha kuwa
katika siku ya kwanza ya mazoezi yao na kikosi hicho wachezaji wote
wameonyesha viwango vya hali ya juu aku akimsifia mchezaji mshambuliaji Akuffo ni hatari
mno na kwa haraka haraka hakuna wa kumfananisha naye kati ya washambuliaji wote
waliopo Tanzania kwa sasa.
Alisema kuwa na uwezo
mkubwa wa kumiliki mpira, kasi, nguvu, ufundi na mbinu za kimchezo maana yake
Wekundu wa Msimbazi wamepata kiongo mwenye vigezo.
Wachezaji wengine wa kigeni
kwenye kikosi cha Simba SC ni washambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na
Mzambia Felix Sunzu ambapo kwa upande wa mchezaji okwi yeye anatarajiwa
kuwasili kambini kesho