BREAKING NEWS

Wednesday, August 29, 2012

WATOTO YATIMA 300 WAPATIWA MSAADA WA FEDHA ZA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO


MWANGA wa matumaini umeng'ara kwa watoto yatima 300 waishio katika mazingira magumu wa shule ya New Vision iliyopo Kata ya Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara watapatiwa fedha za msaada baada ya zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro.

Hayo yameelezwa juzi na Mkurugenzi wa kampuni ya Tanzanite Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya TanzaniteOne Hayley Henning kwenye ziara ya waandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Liquidattion Channel walipotembelea shule hiyo.

Henning alisema kupitia kundi la waandishi wa habari hao kutoka Marekani ambao hutangaza madini ya vito ikiwemo Tanzanite kwa njia ya mtandao watapanda mlima Kilinjaro na kuchanga fedha ili kuwasaidia watoto hao.

Mkurugenzi huyo alisema wameamua kutoa msaada huo utakaotokana na pesa zitakazopatikana katika zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro na pia wamewapa watoto hao zawadi mbalimbali ikiwemo kamera za kisasa.

Pia Henning alisema kuwa kupitia TanzaniteOne,shule ya New Vision itasaidiwa kukamilishiwa ujenzi wa madarasa na mabweni ambao ulishaanza katika kiwanja kinachomilikiwa na Mkurugenzi wa shule hiyo,Rachel Kinariki.

“Tanzanite Foundation tumeanza kampeni za upandaji mlima Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni mama ya TanzaniteOne na fedha zitakazopatikana zitatumika kuwasaidia ninyi wanafunzi na walimu kupunguza changamoto zinazowakabili,” Henning.

Naye Rais wa Liquidattion Channel (LC) Gerald Tempton ambaye aliambatana na wanahabari watano,alisema kuwa wameamua kuwasaidia watoto hao yatima kwa kutoa fedha ambazo zitapatikana baada ya kupanda mlima Kilimanjaro.

“Sisi washirika wa TanzaniteOne wa kuyatangaza madini haya yanayopatikana eneo hili pekee duniani hatukubaki nyuma na tutawachangia dola 10,000 za Marekani  zitsakazowasaidia watoto hawa wa New Vision,” alisema Tempton.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa New Vision Rachel Kinariki alisema anatoa shukrani kwa tukio hilo la kihistoria ambacho kitasaidia watoto hao kufikia hatua moja zaidi ya kuhitaji huduma mbalimbali muhimu.

Ofisa uhusiano wa kampuni ya TanzaniteOne Halfani Hayeshi alisema kuwa kampuni ya TanzaniteOne ndiyo itakayosimamia matumizi na manunuzi ya vifaa,usimamizi wa ujenzi wa umaliziaji wa madarasa na kufikia ukabidhianaji.

”Mchakato wa kupata andiko la mraidi (BOQ) kwa ajili kuendeleza  na kumalizia ujenzi wa madarasa ya shule umeishakamilika na tunajipanga kulisimamia zoezi hili na hatimaye kukabidhi shule,” alisema Hayeshi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates