kikosi simba kipya
Kambi ya Simba imepata pigo baada ya mshambuliaji wake hatariwa kimataifa kutoka Zambia Filex Momba Sunzu kufiwa na dada yake hali inayosababisha kuondoka kambini kwenda kuhudhuria msiba huo mzito
Taarifa iliyotufikia na kuthibitishwa na msemaji wa timu ya Simba Ezekiel Kamwaga imesema Sunzu alipata taarifa za msiba juzi usiku ikiwa ni saa chache baada ya kutoka kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya Simba na Mathare United ya Kenya mchezo ambao Simba ilishinda 2-1
‘Ni kweli Sunzu amefiwa na dada yake aliyefia huku Lubumbashi ambako alikua akiishi na kaka mkubwa wa Filex Sunzua anayecheza soka la kulipwa nchini humu’alisema Kamwaga na kuongezea kuwa kwa sasa utaratibu wa safari unafanyika na huenda akawa nje ya kambi kwa zaidi ya wiki moja
Kufuatia kufiwa na kuondoka kwa Sunzu kambi ya Simba inajikuta ikipwaya kwa kuwa iko katika maadalizi ya mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Azam mchezo utakaofanyika September nane mwaka huu katika uwanja wa taifa jijini dare s salaam.Simba wamethibitisha Sunzu ataukosa mchezo huo
Mwandishi wa gazeti hili alipofika katika kambi ya Simba iliyopo katika hotel ya Briston mjini hapa alishindwa kuonana na mchezaji huo kwani wakati huo alikuwa amejipumzisha chumbani kwake na kusema hayuko tayari kuzungumza lolote
Taarifa za awali zinasema shughuli za mazishi za dada huyo wa Sunzu huenda zikafanyika mjini Lubumbashi alikofia kwani kaka wa marehemu amewekeza mjini humo
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia