MAVETERANI USHIRIKA KUZURU MOMBASA

KLABU ya soka ya Ushirika veterani iko kwenye maandalizi ya safari yao
ya kuelekea  Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya michezo  miwili ya
kirafiki itakayofanyika Septemba 8 na 9 mwaka huu katika uwanja wa
Bandari.

Mweka hazina wa klabu hiyo Jafary Kihango alisema timu hiyo hivi sasa
imeanza kujifua na  mazoezi  katika uwanja wa chuo kikuu kishiriki cha
ushirika na biashara cha Moshi huku akitoa wito kwa wachezaji wengine
wa klabu hiyo kuhudhulia mazoezi.

Alisema timu hiyo inaenda Mombasa kwa mualiko wa klabu ya soka ya
Bandari (KPA)ambako itacheza mchezo wa kwanza na timu hiyo Septemba 8
na mchezo wa mwisho utakuwa ni kati ya Ushirika veteran na timu ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Banandari.

Kihango alisema lengo la safari hiyo ni kuimarisha mahusiano baina ya
timu hizo mbili pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria
ikiwemo ngome ya Fort Jesus ambayo ni maarufu kwa kuwa ni moja ya
vivutio vikubwa nchini Kenya.

Alisema safari hiyo ambayo inakuwa ni ya tatu inafadhiliwa na
wanachama kumi wa  klabu hiyo ya wazee maarufu kama ma cancellers wa
klabu ambapo jumla ya wachezaji 25 na viongozi watatu watafanya safari
Septemba 7 mwaka huu.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia