ZAIDI ya sh350 milioni zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kuanzia Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu kwenye Kata ya Orkesumet Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Akizungumza na Waandishi wa habari Diwani wa kata ya Orkesumet Naftal Ole Peshut alisema miradi iliyotekelezwa imehusisha maeneo ya sekta ya uzalishaji mali,uwezeshaji wananchi,huduma za jamii,miundominu na huduma za uchumi.
Ole Peshut alisema sekta ya elimu imegharimu zaidi ya sh81 milioni,afya sh146 milioni,maji sh549,000 mifugo sh11 milioni,barabara sh76 milioni na ajira na uwezeshaji wananchi sh35 milioni.
Alisema sekta ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi umefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi kufungua akaunti benki ya NMB na kuchukua mikopo kwa kuanzia sh500,000 hadi sh20 milioni.
“Pia wananchi wengi wamehamasika kujiunga kwenye ujasiriamali kwani katika kata yangu kuna vikundi viwili vya chama cha kuweka na kukopa Saccos na vikundi nane vya benki za jamii vijijini Vicoba,” alisema Ole Peshut.
Alisema kwa upande wa sekta ya mifugo wananchi wamehamasika kuchanja mifugo huku wakitakiwa kufuata kanuni ya ufugaji bora na huduma nyingi za chanjo ya mifugo zinapatikana kwa urahisi.
Diwani huyo alisema kuwa ufanisi wa miradi hiyo imetokana na utekelezaji wa Serikali iliyopo madarakani katika kutekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM kwa mwaka 2010 hadi 2015.
Hata hivyo,alisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji kwani kwenye kata hiyo kuna visima vitatu ambavyo viwili vimechimbwa na halmashauri ya wilaya hiyo na kimoja kimechimbwa na taasisi binafsi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia