MAKARANI WA SENSA WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU

Makarani waliohitimu mafunzo kwa ajili ya ukusanyaji taarifa za sensa wametakiwa kuwa na nidhamu nzuri kwa viongozi walioko katika maeneo yao ya kazi ya uhesabuji watu pamoja  na kutanguliza uzalendo katika shughuli hiyo kitaifa.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Karatu mh,Daudi Felex Mtibenda wailayani karatu alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 11 ya makarani wa sensa kiwilaya yaliyoanza ougost 9 mwaka huu.

Mtibenda alianza kwa kuwashukuru makarani hao kwa kuwa wavumilivu katika mafunzo hayo  hasa pale posho zao zilipochelewa kwa zaidi ya siku saba na kupelekea kuishi katika mazingira magumu wakati  wa mafunzo hadi walipopata fedha zao.

"Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa uvumilivu wenu mliouonesha kwa siku saba za mwanzo pale malipo yenu yalipochelewa na hii inadhiirisha kuwa ni uzalendo wa hali ya juu sana na hesima kwa wilaya yetu ya Karatu hivyo muendelee kuwa na moyo huohuo hata katika maeneo mtakayopangiwa ikiwemo kuonesha nidhamu ya hali ya juu kwani itawasaidia kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi hao" alisema Mtibenda.

 Mtibenda aliongeza kuwa mbali na kuwaheshimu viongozi wa maeneo watakayopangiwa katika zoezi la uhesabuji watu hasa viongozi wa serikali, pia aliwataka kuwaonesha wananchi hao nidhamu hiyo ili kuwarahisishia zoezi hilo kwa kupewa ushirikiano wa kutosha kupata takwimu sahihi.

Mkuu huyo pia aliwataka makarani hao waliohitimu mafunzo hayo kuzingatia masomo waliyofundishwa katika kutenda kazi hiyo pamoja na kuzingatia kiapo cha kutunza siri za watu kwanio zoezi hilo ni la kitaifa hivyo wawe wasiri ili kufanikisha kazi muhimu kwa amendeleo ya taifa letu.

"Mwisho naomba nimalizie kwa kuwasisitizia wananchi wa wilaya ya Karatu kuonesha ushurikiano wao wa hali ya juu katika kufanikisha zoezi hili kwa kuwa tayari kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa watakaowatembelea kwani mafanikio ya zaezi hilo ni mafanikio ya Wilaya ya Karatu na Tanzani kwa ujumla.

Awali kabla ya hutuba hiyo, wahitimu hao wa zoezi la sensa 600 waliapa kuifanya kazi hiyo kwa moyo wate na kazi zingine za kitaifa zitakazokuwa mbele yao kwa usiri mkubwa na kutanguliza uzalerndo mbele kwa mafanikio ya nchi yao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post