Mahakama mjini Kigali, Jumatano ilikataa ombi la kumwachia kwa dhamana mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Jean Uwinkindi kutokana na kilichoelezwa na mahakama hiyo kuwa ‘’uzito wa mashitaka anayokabiliwa nayo na wasiwasi kwamba huenda atatoroka.’’
Mchungaji Uwinkindi anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi.Inadaiwa kwamba mchungaji huyo alihamasisha na kuongoza mauaji dhidi ya Watutsi katika parokia yake ya Kayenzi wakati wa mauaji hayo mwaka 1994.
Mchungaji Uwinkindi alitiwa mbaroni Juni 30, 2010 nchini Uganda na kuhamishiwa makao makuu ya ICTR, mjini Arusha, Tanzania, siku mbili baadaye.Aprili 19, 2012 akawa mshitakiwa wa kwanza wa ICTR, kesi yake kuhamishiwa nchini Rwanda kwenda kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo. Alikana tuhuma zote dhidi yake.
Baada ya Jaji John Byakatonda kuamuru kwamba mshitakiwa ataendelea kukaa rumande kwa siku 30 zaidi, Wakili kiongozi wa mshitakiwa huyo, Gatera Gashabana alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia