WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA HASWA KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU

serikali na wananchi wote kwa ujumla wametakiwa kupunguza matumizi mabaya ya fedha hasa siku za sikukuu badala yake wawakumbuke watu wenye mahitaji muhimu kama watoto yatima.

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha living water children center Anzaameni Kimaro kilichopo kata ya Baraa wakati alipokuwa akipokea msaada wa chakula kwa ajili ya sikukuu ya Iddy cha watoto waishio kituoni hapo  kutoka kwa Meya wa jiji la Arusha Gaudience Lyimo.

Bwana Kimaro alianza kwa kuishukuru halmashauri ya jiji la Arusha kupitia Mea wa jiji hilo kwa kuwakumbuka watoto hao yatima katika kuwafanikishia kusheherekea sikukuu hiyo ya Iddy kwani kwa kufanya hivyo kunawafanya watoto hao kujiona wa muhim pindi wanaposherekea sikukuu hizo kamawatoto  wengine wanaoishi na wazazi wao.

Aidha aliwataka wananchi wengine kupunguza matumizi mabaya ya fedha kwa anasa mbalimbali hasa siku za sikukuu badala yake wajitolee kuwasaidia watoto yatima hasa waishio katika vituo lengo ikiwa ni kujipatia baraka kupitia misaada yao badala ya kujiongezea dhambi.

Nae mlezi wa watoto hao bi. Dorah Mtangi alisema kuwa katika kituo hicho kuna watoto 133 wenye umri wa miak tofauti tofauti huku wengine wakisoma shule za sekondari na wengine za misingi pamoja na wengine wadogo wanaolelewa nyumbani.

Aliongeza kuwa "katika kituo hicho hakuna muhisani yoyote bali watu hujitokeza kama kuitwa na Mungu kuja kuwasaidia watoto hawa na wakati mwingine tuna wakati mgumu pale tunapoishiwa na mahitaji muhimu ya watoto hao hivyo wahisani na wananchi kwa ujumla wajitokeze kuwasaidia watoto hoa kwani hali hiyo hawakuiomba bali wamejikuta nayo bala kupenda"

Aidha Meya wa jiji la Arusha alipokuwa akiongea na walezi hao alisema kuwa lengo la kutoa masaada huo ni kusherehekea sikukuu ya Idd na watoto yatima ikiwa ni sehemu ya majukumu yake katika kuihudumia jamii.

Kwa mujibu wa afisa habari wa manispaa ya jiji hilo Ntagenjwa Hoseah alisema kuwa msaada huo uligharimu jumla ya shilingi laki saba kwa kununua sukari, mchele, mafuta nyama,juisi na n.k.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post