SIMBA KUWEKA KAMBI YA KUDUMU A-TOWN

Uongozi wa klab ya soka ya iamba ambao ni mabingwa wa kandada Tanzania bara umeazimia kuweka kambi ya kudumu mkoani Arusha kila inapokua ikijiandaa na mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo ligi kuu ya Tanzania bara
Simba wamefikia hatua hiyo baada ya kuona arusha kuna hali ya hewa nzuri na ushirikiano mmzuri baina ya wanachama na wapenzi wa samba mkoani Arusha na isitoshe mara nyingi Simba hupata mafanikio kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiweka kambi yake mjini hapa
Akizungumza na gazeti hili jana baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya simba na Mathare united ya Kenya makamu mwenyekiti wa simba Geofrey Nyange ‘kaburu’ alisema kimsingi simba imeamua kubaki kambini Arusha hadi kuanza kwa msimu wa ligi September 15 mwaka huu na itacheza mchezo mmoja zaidi wa kirafiki kabla ya kucheza na Azam mechi ya ngao ya jamii kuashiria kuanza kwa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara
SImba imepiga kambi kwa zaidi ya wiki tatu sasa mjini Arusha na chini ya kocha wake Mserbia Milutin Circovic akiwa na kikosi kamili kilichosheheni nyota wa Tanzania  wakiwemo wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa msimu huu kutoka Kenya, Mali, Uganda na Ghana
Wachezaji hao waliwika vilivyo kwa Mghana Daniel Akoufo kuifungia simba goli katika mechi yake ya kwanza bao lililokuwa chachu ya ushindi wa simba, beki Pascal Ochieng kutoka Kenya alionekana kuwa kizingiti kwa washambuliaji wa Mathare utd na raia wa Mali  Komabil Keita akionekana kuziba pengo la Kelvin Yodan aliyetimkia Yanga.
Hata hivyo Keita aliumia katika kipindi cha kwanza na kutoka nje na nafasi yake kuzibwa na Juma Saidi Nyoso
Nyota hao wote walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mathare Unite ya Kenya na kuonyesha viwango vya juu vilivyowaridhisha wanachama na wapenzi wa simba .Mchezaji pekee aliyekosekana katika mchezo huo ni mshambliaji Emanuel Okwi ambaye alikuwa nchini kwao Uganda akiitumikia timu yake ya taifa
Hata hivyo Kaburu amesisitiza mchezaji huyo anarejea nchini leo jumanne na atakwenda moja kwa moja kambini arusha kujiandaa na msimu wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post