BREAKING NEWS

Thursday, August 30, 2012

UVCCM MANYARA WAPAMATA MILIONI TANO KWENYE HARAMBEE

JUMLA ya sh5 milioni zimepatika kwenye harambee ya mfuko wa Umoja wa
Vijana wa CCM (UVCCM) wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
ulioanzishwa na Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo Kiria Laizer.

Fedha hizo zilipatika jana baada ya kufanyika uchaguzi wa UVCCM wa
wilaya hiyo katika ukumbi wa Manyara Inn mji mdogo wa Mirerani na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo walioshiriki pia
kuchangia harambee hiyo.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa
wilaya hiyo Laizer alisema anazindua mfuko wa jumuiya hiyo kwa yeye
kuchangia sh1 milioni na viongozi na wanachama nao wakachangia sh4
milioni.

Msimamizi wa uchaguzi huo,Jamila Mujungu ambaye pia ni Katibu wa CCM
wa wilaya hiyo alisema Laizer amefanikiwa kutetea nafasi yake ya
Mwenyekiti wa UVCCM kwa kupata kura zote 109 zilizopigwa na wajumbe wa
mkutano huo.

Alisema Jackline Momo na Julius Abraham walichaguliwa kuwa wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa na Bakari Matambi,Innocent Vitalis na
Tingidaa Sungare walichaguliwa kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.

Alisema wajumbe wa Baraza la vijana wilaya ni Jane Adison,Lee
Shinini,Mardadi Muna na Kulunju Pariti,mwakilishi wa halmashauri ya
CCM wilaya ni Nina Ole Sendeke na Helena Jackob alichaguliwa
mwakilishi wa kwenda UWT.

Mujungu aliwatangaza wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji wa UVCCM
wilaya ni Jackline Momo,Lee Shinini na Mardadi Muna na Upendo Mwaisomo
alichaguliwa kuwa mwakilishi wa UVCCM jumuiya ya wazazi wilaya.

Naye,mgeni rasmi wa mkutano huo wa UVCCM,Jackson Sipitek ambaye pia ni
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro aliwataka
vijana wa wilaya hiyo kutangaza maendeleo mbalimbali yaliyofanywa na
Serikali.

“Serikali iliyopo madarakani inatokana na Chama Cha Mapinduzi hivyo
vijana mna haki ya kutembea kifua mbele na kutangaza mafanikio
yaliyopatikana kuliko kukaa kimya na kuwapa sauti wapinzani wa CCM,”
alisema Sipitek.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates