Zaidi ya miradi 51 ya maendeleo
ya wananchi itazinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa
mwaka huu, kepteni Ernest Mwanosa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 mkoani Kilimanjaro.
Akikabidhiwa mwenge wa uhuru ukitokea mkoa wa Manyara mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,
alisema kuwa mwenge huo utazindua miradi
yote iliyopo kwenye halimashauri saba za mkoa.
Gama alieleza kuwa miradi
hiyo imegusa sekta zote muhimu ambazo ni miradi ya Afya, maji, kilimo mifugo na ushirika, miundombinu hifadhi ya
mazingira, biashara na ujasiria mali.
Alisema alisema miradi
mingine ni Elimu na utawala na miradi mingineyo, na kueleza kuwa mbio za mwenge
zitaimarisha na kuibua upya ari ya
kupambana na madawa ya kulevya, rushwa naelimu juu ya umuhimu wa sensa ya watu
na makazi.
Gama alisema kuwa mkoa wa
Klimanjaro unakabiliwa na changamoto kubwa ya usambazaji na matumizi makubwa ya
madawa ya kulevya kutokana na mkoa kupakana na
nchi jirani ya Kenya pamoja na kuwepo kwa uwanja wa Ndege wa kimataifa
wa Kia.
Alisema kutokana na kuwapo
kwa changamoto hiyo, serikali kupitia jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele
katika mambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya, ambapo jumla ya watu
1,243 wamekamatwa kuhusika na matumizi na usambazaji wa dawa hizo.
Kwa upande wake kiongozi wa
mwenge kitaifa, Ernest Mwanosa, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano katika
kushiriki kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi litakaloanza Agost 26 mwaka
huu, kwa lengo la kuipa serikali uraisi wa kuleta maendeleo wa urahisi.
Mwanosa aliwataka wananchi
kutambua kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kila mtanzania,
kwa serikali kupata takwimu za watu itarahisisha zaidi kubaikna kwa mahitaji ya
maendeleo.