JESHI LA POLISI LAAMUA KUSIKILIZA KILIO CHA WANANCHI WA MBUGUNI

SIKU chache baada ya mbunge wa viti maalumu mkoani Arusha,Rebeca Mgondo kupigia kelele bungeni tatizo la uhaba wa askari wa kike katika kituo cha polisi cha kata ya Mbuguni jeshi la polisi mkoani Arusha limewapeleka “chap chap”askari watatu wa kike katika kituo hicho.

Hivi karibuni mbunge huyo  akitoa mchango wake bungeni alilalamikia kitendo cha jeshi la polisi nchini kushindwa kupeleka askari wa kike katika kituo hicho kitendo kinachopelekea baadhi ya wanawake wanaokamatwa na  kufikishwa kituoni hapo kupekuliwa na askari wa kiume kitendo alichodai ni udhalilishaji wa kijinsia.

Hatahivyo,baadhi ya wananchi wa kata ya Mbuguni wamemwagia sifa mbunge huyo wa viti maalumu  kwa kupigia kelele  tatizo hilo na hatimaye serikali kusikiliza kilio hicho huku wakimsihi ya kwamba wako pamoja naye katika harakati zake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolfikia libeneke hili zindai ya kwamba mara baada ya mbunge huyo kulalamikia kitendo hicho jeshi la polisi mkoani hapa liliamua kuwapeleka askari watatu wa kike kwa lengo la kutoa fursa na haki kwa wananchi wa kada zote.

Taarifa hizo zimedai ya kwamba askari hao waliletwa katikati ya mwanzoni mwezi Agosti mwaka huu na kisha kuripoti katika kituo hicho kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.

Kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya suala hilo alikiri askari hao kuripoti katika kituo hicho lakini alisema kwamba wameripoti kwa mujibu wa taratibu za jeshi la polisi na si vinginevyo.

“Hilo suala lilishafungwa na mjadala wake ulishafungwa askari wameripoti kwa mujibu wa taratibu za jeshi la polisi na si vinginevyo”alisema Sabas bila kutaja majina ya askari hao

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo waliohojiwa kwa nyakati tofauti na libeneke hili walimwagia sifa mbunge huyo kwa kupigia kelele suala hilo ambalo walidai kwamba ilikuwa ni kero ya muda mrefu.

Bila kutaja majina yao hadharani walisema kwamba wanamshukuru mbunge huyo kwa kutetea kilio chao bungeni na hatimaye serikali kutimiza wajibu huo huku wakimsihi ya kwamba wapo naye bega kwa bega katika harakati zake.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post