MJANE ,Ruth Timotheo mkazi wa kata ya Mbuguni
wilayani Arumeru Mashariki amejikuta akiangua kilio mbele ya mbunge wa
viti maalumu mkoani hapa kupitia Chadema,Rebeca Mgondo akilalamikia uongozi
wa shule mojawapo ndani ya kata hiyo sanjari na baadhi ya viongozi wa
serikali ya kijiji cha mbuguni kuwa wamepanga njama za kutaka kumpora
ardhi ya shamba lake ambayo aliachiwa urithi na marehemu mme wake .
Mjane,huyo alitoa madai
hayo mbele ya mbunge huyo wa viti maalumu mkoani hapa wakati
alipotembelea eneo la shamba hilo lenye ukubwa wa ekari moja alilodai
kuachiwa kama sehemu ya urithi na marehemu mume wake,Timotheo Nganaeli.
Akitoa maelezo yake
mbele ya mbunge huyo,mjane huyo alisema ya kuwa hivi karibuni vijana
watano wasiofahamika walivamia katika shamba lake na kisha kukata migomba na
mazao mbalimbali kwa madai kuwa wametumwa kungo”a mbegu na kiongozi wa shule
hiyo.
Alisema kuwa vijana hao
walimweleza ya kuwa shamba hilo si mali yake kwa kuwa limeshauziwa kwa shule
hiyo na mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia huku wakitishia kumtoa roho
endapo akiendelea kung”ang”ania shamba hilo.
“Walisema wametumwa
kungo”a mbegu kwenda kupanda kule chini waliniambia kuwa shamba si la kwangu
kwa kuwa limeshanunuliwa kwanini wananinyanyasa hivi jamani”alisema huku
akiangua kilio
Huku akizungumza kwa
huzuni mbele ya watoto wake mjane huyo alisema kuwa mara baada ya tukio hilo
alijitahidi kufika katika kituo cha polisi cha Mbuguni kwa lengo la kutoa
taarifa lakini alijikuta akinyimwa ushirikiano na kuelezwa kurudi kesho
yake kwani wao watamwita mtuhumiwa aliyevamia shamba lake
Alisema kuwa mara baada
ya kuwasili kesho yake kuwasili tena mbele ya kituo hicho kusaka msaada
akiongoza na watoto wake wawili katika hali isiyo ya kawaida alijikuta
akiwekwa ndani ya kituo hicho na yeye na watoto wake ghafla.
“Mara baada ya uvamizi
huu nilienda kituo cha polisi cha Mbuguni kusaka msaada askari wakanijibu kuwa
nirudi kesho kwani watamwita aliyevamia shamba nirudi kesho,na niliporudi kesho
yake nikajikuta mimi na watoto wangu wawili tunaweikwa ndani bila kujua
kwanini”alisema huku akitoa machozi
Hatahivyo,akienda mbali
kusimulia mkasa huo alisisitiza kuwa ilimlazimu kutoa kiasi cha sh,160,000
katika kituo hicho cha polisi kama fidia ya kuachiwa yeye na wanaye huku akimwangukia
mbunge huyo kumsaidia.
Naye,mbunge huyo
alipinga vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu hao kwa lengo la kutaka
kumpora mali yake mjane huyo huku akihaidi kumsaidia kupambana nao
vikali mbele ya vyombo vya sheria .
Diwani wa kata ya
Mbuguni,Thomas Mollel alipotafutwa na gazeti hili hakuweza kupatikana lakini
alipotafutwa kaimu kamnda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Akili Mpwapwa alisema
ofisi yake bado haijapata taarifa hizo na kuhaidi kulifuatilia madai hayo kwa
undani.