Watendaji wa serekali na watanzania
kwa ujumla wametakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yao na kujali maslahi ya utaifa
badala ya kuangalia maslahi binafsi,matokeo yake ni kuwapa wawekezaji uchwara
rasilimali za nchi na nchi kuingia matatizoni.
Akizungumza na wanahabari mkurugenzi
wa NMC mkoani hapa Josephat Mtinange alisema kuwa ni hatari kwa nchi kama yetu
kutawaliwa na ubinafsi badala ya kutanguliza maslahi ya watanzania mbele huku
ni kuuza rasilimali kwa wawekezaji uchwara ambao hawapo kwa maslahi ya
watanzania na kushindwa kuendeleza mashirika yetu.
Mtinange alisema kuwa niabu kwa
watendaji wa serekali kujilimbikizia mali huku ndugu zao wakishindia mihogo ya
kuchoma wakati wengine wakitoa mashirika kwa wawekezaji ambao wameshindwa
kuyaendeleza mashirika yetu na mengine kufa kifo cha mende.
“Watu wana sifa lakini si wazalendo
wamekuwa wakigawa rasilimali za nchi vibaya bila ya kujali maslahi ya wengi na
kuwaacha watanzania katika lindi la umaskini bila ya kujua kesho yao”alisema
Mtinange.
Kwa hili tunakwenda wapi watoto wetu
tunawarithisha nini kila mtu ameweka ubinafsi mbele kwa maslahi yake siyo ya
taifa kwa mfano mashirika kama haya yameuzwa kwa bei poa kwa wawekezaji bila ya
kuangalia kama yanaweza kujiendesha au la.
Alisema kuwa mashirika kama hayo
yamewekwa kwa muuzaji consolidated holding corporation(CHC) Huku yanauwezo wa
kujiendesha na wala hayadaiwi na mtu huku ni kuikosesha serekali mapato ya
viwanda kama hivi.
Utakuta mashirika mengi ya umma
yamebinafsishwa lakini hayajaendezwa na wawekezaji kwa kuyafanya magodown huku
ni kuwakosesha ajira watanzania tufike mahali tukemee hayo kwa nguvu zetu zote
kama kweli tunauchungu na nchi hii.
Wakati wa baba wa taifa mwl. Julius
Nyerere alitufundisha kuwa tusikubali kuwa watumwa kwa vibaraka wachache kwa
maslahi yao binafsi na kuangali utaifa kwanza bila ya kuogopa na hili mwalimu
alilisimamia ipasavyo leo nchi yetu inaheshimika kote ulimwenguni kwa misimamo
yake.