CHADEMA WAMSHUKIA SENDEKA JIMBONI KWAKE, WAVUNA WANACHAMA 1,200
Lema akipokea kadi za wanachama wapya simanjiro
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na operesheni yake ya
“Vua Gamba Vaa Gwanda” ambapo juzi walifanikiwa kuvuna zaidi ya
wanachama 1,200 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka maeneo mbalimbali
ya wilaya ya Simanjiro.
Operesheni
hiyo iliyoendeshwa kwa kutumia usafiri wa helkopta (chopa) na magari
iliongozwa na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Godbless Lema
akishirikiana na aliyekuwa mwenyekiti wa UV CCM mkoani Arusha, James
Olle Millya ambaye ni mwenyeji wa Simanjiro mwenye ushawishi mkubwa kwa
watu wa wilaya hiyo.
Wanaccm
hao walirudisha kadi pamoja na sare mbalimbali za chama hicho zikiwemo
flana zilizokuwa na picha ya mwenyekiti wao wa Taifa, Rais Jakaya
Kikweta, bendera na vitambaa vya kichwa kwenye maeneo ya Narekauo, Lolbosiret, Naberera, Ndovu, Orkesument na Marerani ilikofanyika mikutano hiyo iliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Akizungumza
kwenye mikutano hiyo Lema aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu kutoa
maoni yao kwenye Tume ya Katiba pindi itakapopita kwenye maeneo hayo
ili kuhakikisha kero zao zinapatiwa ufumbuzi kupitia katiba mpya ikiwemo
kuhakikisha utitiri wa viongozi wasio na majukumu kwenye mfumo wa
serikali unaondolewa ikiwemo nafasi za wakuu wa wilaya na mikoa ambao
wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi wanayofanya zaidi ya
kupeleka maneno “umbea” kwa viongozi wa juu.
Aidha
alilitaka jeshi la polisi kumuhoji Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusiana
na sakata la kutekwa Dk. Steven Ulimboka kwa kile alichodai kuwa
kunauwezekano akawa anawajua watekaji hasa kutokana na kauli aliyoitoa
bungeni siku moja kabla ya kiongozi huyo wa madaktari nchini kutekwa na
kuumizwa vibaya aliyosema kuwa liwalo na liwe.
Lema
alisema kuwa jeshi la polisi linatakiwa kufanya kazi kwa weledi
likizingatia sheria hasa katika tukio hilo linalogusa hisia za wengi na
wapenda demokrasia kwani hakuna aliye juu ya sheria hivyo waziri mkuu
ahojiwe ili kuweza kubaini kilichokuwa nyuma ya kauli yake hiyo.
Alisema
kuwa ni vema mfumo wa kupata mawaziri ukabadilishwa kwa watu kuandika
barua za maombi badala ya sasa ambapo viongozi hao hupatikana kwa
kuteuliwa na rais miongoni mwa wabunge jambo linalopekea utandaji wa
serikali kuwa duni huku wananchi wakisidi kusongwa na kero mbalimbali
bila kupatiwa utatuzi.
Lema
ambaye alikuwa mbunge wa Arusha Mjini kabla ya mahakama kumvua mapema
mwezi aprili mwaka huu, alishauri ni vema mfumo wa kuwapata majaji nao
ukaboreshwa kwa kuwepo na chombo cha kuwateua tofauti na sasa ambapo
huteuliwa na Rais wan chi jambo linalowafanya viongozi hao wa muhimili
wa kutoa haki kutokuwa huru.
Lema
alitumia fursa hiyo kumshambulia mbunge wa jimbo hilo, Christopher
OleSendeka, (CCM), kuwa ni mtu asiye na msimamo huku akimfananisha na
tunda la tikiti maji ambalo nje ni kijani ndani ni jekundu kwa madai
kuwa mbunge huyo ni ndumila kuwili kwani mchana mbunge huyo ni CCM
lakini usiku hugeuka kuwa Chadema.
Alisema
kuwa tabia hiyo ndiyo inayomfanya mbunge huyo wa Simanjiro kushindwa
kutetea maslahi ya wananchi wake ambao wengi wanaishi kwenye lindi kubwa
la umaskini ikiwemo kukosa huduma muhimu za barabara, zahanati, elimu,
afya na maji safi wakati jimbo hilo linahazina kubwa ya utajiri ikiwemo
machimbo ya madini yenye thamani kubwa ulimwenguni ya Tanzanite.
“Asubuhi
nimefanya mkutano kwenye kijiji cha Ndovu, nikaona wananiletea chupa ya
maji mwanzo nilidhani wananipa dawa lakini nilisikitika wananchi wale
waliponiambia maji hayo ndiyo wanayoyatumia kwa ajili ya kunywa toka
kwenye kisima wanachochangia na mifugo, hii ni hatari sana kwa afya zao,
ninawasiliana na wabunge wa Chadema ili wayapeleke bungeni, hivi kwenye
maisha haya yanawastahili wananchi wanaoishi kwenye utajiri mkubwa wa
Tanzanite?” alihoji Lema.
Kwa
upande wake Millya aliwataka wananchi wa Simanjiro kuungana naye kwa
kuhamia Chadema ili waunganishe nguvu katika harakati ya kudai haki zao
ikiwemo kupigania kunufaika na madini ya Tanzanite yanayopatikana ndani
ya wilaya hiyo kwani CCM kwa miaka 50 imekuwa ikitoa ahadi nyingi za
neema kwa wananchi hao lakini hawazitekelezi.
Aliwataka
wasitishike na vitisho wanavyotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM
kwenye eneo hilo ambao wananchi walimweleza kuwa siku moja kabla ya
mkutano huo walipita kwenye kila boma(familia) wakiwataka wananchi
wasijitokeze kwenye mkutano huo lakini wananchi wakawapuuza na
kujitokeza kwa wingi.
Aliwataka
wananchi hao kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuwagawa kwa kigezo cha
wenyeji na wakuja kwa kile alichodai kuwa lengo la watu hao siyo zuri
kwani Watanzania wanahaki ya kuishi kwenye eneo lolote hapa nchini
hivyo waendelee kushirikiana katika kujiletea maendeleo na kupigania
haki zao kwa pamoja.
Millya
alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa wakati Taifa likifikisha miaka 50
ya uhuru lakini mpaka sasa wananchi wa jamii ya kimaasai bado
wananyanyaswa na kuwa kama ombaomba wa ardhi kutokana na kutopewa ardhi
ya kutosha kwa ajili ya shughuli zao za ufugaji na makazi.
Viongozi
wengine walihutubia kwenye mikutano hiyo ni pamoja na aliyekuwa diwani
wa Sombetini kwa tiketi ya CCM ambaye hivi karibuni alihamia Chadema,
Alphonce Mawazo na aliyekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa CCM na
UVCCM, Ally Bananga.
habari kwa hisani ya habari Tanzania
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia