ATAKA WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AACHIWE HURU
Wakili
wa utetezi katika kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa Mipango ,
Augustin Ngirabatware Jumatano aliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji
ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kumwachia huru mteja wake kwa madai kwamba
mwendesha mashitaka ameshindwa kuthibitisha mashitaka pasipo mashaka.
‘’Ushahidi
uliotolewa na Ngirabatware ni zaidi ya ushahidi wa kuaminika na
umeonyesha zaidi ya vigezi vya kuwepo mashaka katika kesi ya mwendesha
mashitaka hivyo hamna budi kumwachia huru,’’ Wakili Kiongozi, Mylene
Dimitri aliiambia mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji William Sekule.
Dimitri
ambaye alikuwa anatoa hoja za mwisho katika kesi ya mteja wake alidai
kwamba ushahidi wa Ngirabatware kuwa kamwe hakushiriki katika mauaji
dhidi ya Watutsi katika wilaya ya Nyamyumba, mkoa wa Gisenyi, Kaskazini
mwa Rwanda alikozaliwa ulikuwa ‘’ wenye maana, haikuegemea upande wowote
na wa kuaminika kwa kiwango cha hali ya juu,’’
Wakati
wa usikilizaji wa kesi yake, Ngirabatware alitoa sababu kadhaa kwamba
hakuwapo nyumbani kwao wakati uhalifu ulipokuwa unafanyika. Alidai
kwamba kati ya Aprili 23 na Mei 23, 1994, alikuwa katika safari za
kikazi katika nchi mbalimbali zikiwemo, Senegal, Gabon na Uswisi.
Lakini
kwa upande wake mwendesha mashitaka alikuwa na maelezo tofauti kuwa
katika kipindi hicho, mshitakiwa alikuwa mkoani Gisenyi, hususan ni
katika wilaya yake ya Nyamyumba akidaiwa kushiriki katika kutenda
uhalifu huo.
Kwa
mujibu wa wakili huyo, Ngirabatware aliwasilisha nyaraka kadhaa
kudhibitisha hoja zake ikiwa ni pamoja na hati yake ya kusafiria
zikionyesha tarehe mbalimbali alizosafiri na viza alizopewa, mahojiano
na vyombo mbalimbali vya habari na barua kutoka balozi mbalimbali
zikionyesha kutokuwepo kwake nchini Rwanda wakati huo.
Hata
hivyo wakati wa kuwasilisha hoja za mwisho, mwendesha mashitaka alidai
kwamba ushahidi wa kutokuwapo nchini Rwanda uliotolewa na mshitakiwa
umepingana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wake mwenyewe na wa
mwendesha mashitaka.
Mwendesha
Mashitaka Wallace Kapaya alifafanua zaidi kuwa mashahidi wa utetezi
waliotoa ushahidi kuunga mkono hoja ya mshitakiwa, walikuwa marafiki
zake wa karibu au jamaa zake hivyo, wana lengo la wazi kabisa la kutaka
kumnusuru mshitakiwa. Alidai pia kwamba tarehe zilizoonyeshwe kwenye
hati ya kusafiria zimegushiwa.
‘’Kutokana
na kupinga huko kwa wazi na urafiki wa mashahidi hao na mshitakiwa,
nawaomba muukatae ushahidi huu,’’ Kapaya alisisitiza.
Pande
zote mbili za mwendesha mashitaka na utetezi zilihitimisha kuwasilisha
hoja za mwisho na kesi kuahirishwa kwa muda usiojulikana.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia