SEREKALI YATAKIWA KUTOA TAMKO LA WATU WAVURUGAO AMANI
UMOJA
wa makanisa Arusha na Kanda ya Kaskazini umesema kuwa kitendo cha
serikali kutoyakuchukulia hatua makundi yanayoendesha harakati za
kuvuruga amani nchini kinaonyesha kuwa serikali inakubaliana nayo.
Hayo
yalisemwa jumanne na askofu Joseph Mutorela wa kanisa la Monnonite
Tanzania alipokuwa akisoma tamko la pamoja la umoja huo kwenye hoteli ya
Corridor Spring kwenye kikao kilichoudhuriwa na askofu wa KKKT,
dayosisi ya kaskazini kati, Thomas Laizer, Msaidizi wa askofu wa kanisa
la katoliki jimbo kuu Arusha, Simon Tenges, askofu wa Anglikana
daiyosisi ya mlima Kilimanjaro, Stanley Hotay pamoja na wawakilishi toka
madhehebu ya kipentekoste.
Alisema
kuwa kwa nyakati tofauti baadhi ya waislam kupitia mihadhara na vyombo
vya habari wamekuwa wakitoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya
ukristo pamoja na kueneza chuki katika jamii lakini serikali imekuwa
haichukui hatua zozote kudhibiti hali hiyo isiendelee.
“Kwamba
hali ya uchochezi na vitisho imeenda mbali zaidi hadi kuingia katika
uharibifu wa mali na kusitisha uhai wa watu wa Mungu, mfano uchomaji wa
makanisa na uharibifu wa mali Zanzibar mnamo tarehe 26, 27 na 28 may,
2012 na kifo cha mwinjilisti huko Mto wa Mbu februari 24, 2011”
“Wajibu
wa Serikali kusimamia sheria na taratibu za nchi. Hivyo inapoonekana
baadhi ya makundi yakiendelea na harakati zao za kuvuruga amani na
kusababisha hofu bila hatua zozote madhubuti kuchukuliwa kunaleta hisia
kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali wanakubaliana na hali hiyo” alisema
Askofu Mutorela.
Aidha
alidai kuwa kuwa ukimya wa kistaarabu ambao umeendelea kuonyeshwa na
wakristo kwa jinsi yoyote usitafsiriwe kama ujinga wala uoga ambapo
aliwataka Wakristo wote nchini kumuomba Mungu aliye hai ili kusudi lake
likasimame.
Hata
hivyo viongozi hao wa dini hawakukubali kutoa fursa ya kuulizwa maswali
na wanahabari waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo kwa madai kuwa
kwenye ratiba ya hawakupanga kipengele hicho.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia