ZAIDI YA ASILIMIA 90%YA MADEREVA PIKIPIKI AWANA LESENI
![]() |
| Mkijua sheria za usalama barabarani hata rushwa hamtatoa maana unajua sheria |
![]() |
| Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Marson mwakyoma akiongea na baadhi ya madereva wa pikipiki waliofuata pikipiki zao kituoni hapa ambazo zimekamatwa |
ZAIDI ya
asilimia 90% ya madereva wa pikipiki mkoani Arusha hawana
leseni za udereva na wengine hawajui sheria za barabarani
Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani mkoani hapa Marson Mwakyoma wakati akifanya mahojiano na libeneke la kaskazini ofisini kwake
Alisema kuwa kutokana na ajali nyingi ambazo zimekuwa
zikitokea kikosi cha usalama babarbarani kimefanya uchunguzi na kubaini kuwa
zaidi ya madereva hao wamekuwa hawana leseni na
ambao wanayo wamekuwa hawajapata kwakufata sheria na wengine hawajasoma kabisa.
Alisema kuwa ajali kutoka na ajali nyingi ambazo zimekuwa
zikituokea mara mara wameamua kuanzisha operesheni maalumu ya kusaka madereva ambao hawana leseni na
wale ambao hawafati sheria za barabarani na iwapo wanawakamata basi watashika
pikipiki zao na kuziweka ndani hadi pale dereva atakapokuja na cheti kinachoonyesha amesoma .
Alibainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya pikipiki 60
zimekamatwa kutokana na makosa
mbalimbali na madereva wake wamepelekwa katika chuo kimoja wapo cha udereva
kupat aelimu na iwapo watamaliza basi watarudishiwa pikipiki zao.
“ unajua madereva hawa wamekuwa wanalalamika kuwa garama ya
kusoma ni kubwa hivyo tumeamua kuomba chuo kimoja cha udereva kupunguza bei na
madereva hawa ambao watakuwa wamekamatwa wataenda pale kupata elimu hiii
nadhani itasaidi kupunguza ajali nyingi ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara
na kusabishia watu vilema vya maisha na wengine vifo”alisema Mwakyoma
Aidha alibainisha kuwa faini ya shilingi 30000 haisaidii
kitu ila iwapo hawa madereva watafanya kozi hii basi anauhakika ajali za
barabarani zitapungua kabisa na mwishowe
kwisha kabisa na alibainisha kuwa tangu operationi hiyo ianze ajali za pikipiki
zimekuwa zikipungua siku adi siku huku akisema kuwa zoezi hili ni endelevu .
Aliwataka waendesha pikipiki hizi kwenda kusoma kwani
wakijua sheria za barabarani itawasaidia hata ao wenyewe kutotoa rushwa ovyo
kwani iwapo atajua sheria basi hamna askari yeyote atakaye mnyanyasa barabarani
Alitoa wito kwa madereva kwenda TRA kukata tin no kwani
wasipokuwa na tin hawataweza kupata leseni zao huku akisisitiza kuwa tin hizo
zinatolewa bure pasipo kuchajiwa kiasisi chochote cha fedha.


0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia