ATAKA WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AFUNGWE MAISHA
Mwendesha
Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
(ICTR) Jumatatu ameiomba mahakama hiyo kumpatia adhabu ya kifungo cha
maisha jela Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda, Augustin Ngirabatware
iwapo atatiwa hatiani kwa kuhusika na mauaji hayo mwaka 1994.
Akitoa
sababu kwa nini Waziri huyo apewe adhabu kali kiasi hicho, Mwendesha
Mashitaka, Rashid Rashid alisema ‘’kutokana na ushahidi ulitolewa
mahakamani, nia ya Ngirabatware ya kutekeleza mauaji ya kimbari
imethibitishwa pasipo mashaka.’’
Mwendesha
Mashitaka alikuwa anatoa hoja za mwisho katika kesi hiyo, mbele ya
mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji William Sekule. Alifafanua kwamba
Ngirabatware alitenda uhalifu wa kutisha na kushiriki katika njama za
uhalifu huo kwa kushirikiana na watu wengine.
‘’Alitekeleza,
kuandaa,kuchochea, kuhimiza, kusaidia na kupiitisha adhma ya mauaji
dhidi ya raia wa Watutsi.Ametekeleza uhalifu huo katika wilaya
alikozaliwa ya Nyamyumba, mkoa wa Gisenyi, Kaskazini mwa Rwanda,’’
mwendesha mashitaka alisema.
Rashid
alilikumbusha jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo kuwa
walisikiliza ushahidi wa siku moja baada ya kutunguliwa kwa ndege ya
Rais Junvenal Habyarimana Aprili 6, 1994 na kusababisha kifo chake
kwamba mshitakiwa alikwenda wilayani kwake ambako alidaiwa kupeleka
silaha.
Mwendesha
mashitaka iliendeela kufafanua kwamba, Ngirabatware kama Waziri katika
seriklai ya mpito, mjumbe wa chama tawala cha MRND katika ngazi ya mkoa
na mkwe wa mfanyabiashara maarufu, Felicien Kabuga, ambaye ndiye
anayesadikiwa kufadhili mauaji ya kimbari, alikuwa mtu mwenye ushawishi
mkubwa katika wilaya na mkoa wake.
‘’Alihakikisha
kwamba Faustine Bagango, anachaguliwa kuwa meya wa wilaya yake na kuwa
kitivo cha utekelezaji wa mauaji dhidi ya Watutsi. Walikuwa na malengo
sawa. Alimtumia kusambaza silaha pamoja na kupanga na kuwaongoza
wanamgambo wa Interahamwe kuua Watutsi,’’ alieleza.
Rashid aliongeza, ‘’Ngirabatware hakutaka tena kuona Mtutsi yoyote katika wilaya ya Nyamyumba,’’
Waziri
huyo wa zamani anashitakiwa kwa kula njama za kufanya mauaji ya
kimbari, mauaji ya kimbari au kushiriki mauaji hayo, uchochezi,
kuteketeza kizazi na ubakaji kama uhalifu dhidi ya binadamu.
Uwasilishaji wa hoja za mwisho unaendelea Jumanne.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia