TANFOAM ARUSHA WALALAMIKIA KUHUJUMIWA

Magodoro 9 feki ya kampuni nyingine yakiwa na nembo ya Tanfoam yakipakiwa na kampuni ya uwakala ya majembe Action mart katika moja ya operesheri za kutambua bidhaa za tanfoam zinazochakachuliwa na wafanyabishara
Meneja opereshen wa kampuni ya mejembe action mart,bw Mussa Matto alionyesha moja ya magodoro yanayouzwa na wafanyabiashara eneo la mbauda jijini Arusha,yasiyo ya kampuni ya Tanfoam likiwa limewekwa nembo ya Tanfoam

KAMPUNI ya kutengeneza magodoro ya Tanfoam mkoani Arusha imebaini kuhujumiwa kwa bidhaa zake na baadhi ya wafanyabiashara  wajanja wasio waaminifu kwa kutumia nembo inayofanania katika magodoro ya kampuni nyingine na kuyauza kwa kutumia jina la kampuni hiyo.

Akizungumza katika opareshion inayoendeshwa na kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart ya jijiji Arusha,kwa niaba ya Tanfoam ,Meneja Operesheni, Mussa Motto alisema kuwa ,zoezi hilo linafanyika katika mikoa mbalimbali huku lengo likiwa ni kudhibiti wimbi la uchakachuaji wa madogoro ya Tanfoam linalofanywa na baadhi wafanyabiashara.

Alisema kampuni hiyo ilibaini kuwepo kwa magodoro  feki ya Tanfoam na kulazinika kuendesha operesheni ,ambapo hadi sasa zaidi ya magodoro 500 yamekwishakamatwa  yakiwa  yamechakachuliwa na kuwekwa nembo ya Tanfoam huku ubora wake ukionekana hafifu  tofauti na magodoro halisi na kusababisha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wateja wao.

Aliongeza kuwa ,operesheni hiyo imeanzia mkoani kilimanjaro na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya wafanyabiashara huku wengi wao wakifanikiwa kukimbia baada ya kuwepo malalamiko ya wateja wao kulalamikia ubora hafifu uliopo katika  magodoro hayo ndipo walipofikia hatua ya kuweka wakala kwa ajili ya kuthibiti hali hiyo.

Aidha alibainisha kuwa, kampuni hiyo ya Tanfoam imelazimika kuendesha operation hiyo kwa kutumia kampuni ya udalali ya Majembe ambayo imekuwa ikiyakamata na kuyaweka kwenye  godauni  lao  na baadaye kuteketezwa kwa moto.

Alifafanua kuwa wafanyabiashara wamekuwa waitumia mbinu chafu ya kugonga nembo ya Tanfoam kwenye magodoro ya kampuni nyingine na kuyauza kwa bei ile ile ,baada ya kufanikiwa kutengeneza nembo ya muhuri wa moto unaofanania na ule wa Tanfoam.

Alisema ,hali hiyo ni kinyume cha sheria na wamekuwa wakiwaibia wateja kwa kuwauzia bidhaa isiyo haisi huku kampuni ikishindwa kufikia malengo ya mauzo ya bidhaa zake.

‘’Unajua katika biashara yoyote kuna ushindani mkubwa sana wa kibiashara na kila mtu anabuni mbinu ya kutumia  ili kuweza kumudu soko la ushindani, hivyo tumegundua kuwa asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara wamekuwa wakitumia nembo zetu kuuzia magodoro yao ‘’alisema Motto.

Aliongeza zaidi kuwa, operation hiyo ni endelevu na itafanyika katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ,na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa bidhaa hizo feki.

Nao baadhi ya  wakazi wa mbauda jijini Arusha walisema kuwa zoezi la operesheni hiyo liwe endelevu na kutoa wito kwa kampuni  ya Tanfoam kuhakikisha kuwa inadhibiti bidhaa yake ili wajanja wasifanikiwa kuiga.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia