SEREKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IKO KWENYE MCHAKATO WA KUAANDAA SHERIA
Seriklai ya mapinduzi ya Zanzibar imesema iko katika mchakato wa kuandaa sheria itakayosimamia
sera ya mafuta visiwani humo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa waziri wa ardhi nyumba maji na nishati Ramadhana Abdala Shaaban
wakati akiwasilisha hotuba ya makadiro ya mapato na matumizi kwa wiraza yake
kwa mwaka 2012-2013 katika baraza la wawakilishi .
Waziri huyo amesema tayari maandalizi ya sheria
hiyo yamekamilika ambapo itasimamia zaidi masuala ya nishati visiwani humo.
Aidha amesema katika kuimarisha sekta ya nishati
na madini serikali imewapeleka baadhi ya wataalamu nje ya nchi kwaajili ya mafunzo
ikiwemo suala la mafuta na gesi.
Hatua hiyo inakuja wakati ambapo seriklai ya
mapinduzi ya zanziba inasubiri kuondolewa kwa mafuta
na gesi asilia katika masuala ya Muungano .
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia