Serikali wilayani hai imesambaza katiba zaidi ya 200 vijijini
Serikali
wilayani Hai Mkoani Kimanjaro imefanikiwa kusambaza katiba
zaidi ya 200 katika vijiji mbalimbali, tarafa, kata, taasisi pamoja na vyama
vya siasa wilayani humo
Lengo la
hatua hii ni kuwawezesha wananchi wa wilaya ya Hai kuweza kushiriki kikamilifu
katika mjadala wa marekebisho ya katiba
mara tume ya kukusanya maoni itakapokuwa
wilayani Hai
Mkuu wa
Wilaya ya Hai Bwana Novatus Makunga amesema hayo katika mahojiao na mwandishi
wa habari hizi juu ya makakati wa
Serikali katika Wilaya hiyo katika kufanikisha mjadala wa Maoni ya Katiba
Bwana Maunga amesema
Ofisi yake imepeleka katia idara
za Serikali nakala 16 za Katiba , Ofisi za Tarafa katiba
tatu, na Ofisi za Kata katiba 14
Mkuu huyo wa
Wilaya amefafanua kuwa nakala 120 za Katiba zimepelekwa katika Ofisi za Vijiji, nakala 41
zimepelekwa katika madhehebu ya dini, mashirika yasiyo ya Kiserikali yamepatiwa
nakala sita
Aidha Vyama
vya Siasa vimepatiwa nakala saba za katiba ili wananchama wao
waweze kuipitia na kuijadili kabla ya
kutoa maoni mbele ya Tume ya kukusanya maoni itakapokuwa katika Wilaya hiyo.
Amesisitiza Bwana Makunga leo
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia