WALIOACHIWA HURU WATAKA ICTR IWASIKILIZE KUPATA NCHI YA KWENDA KUISHI
Watu
wanne kati ya watano walioachiwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wamemwomba Rais wa Mahakama hiyo
kuunda jopo litakalosikiliza madai yao kuhusu kukosekana kwa nchi ya
kuwapokea.
Watu
hao ni pamoja na mawaziri watatu wa zamani wa Rwanda, Andre
Ntagerura(Usafirishaji), Jerome Bicamumpaka (Mambo ya Nje) na Casimir
Bizimungu (Afya) pamoja na Brigadia Jenerali Gratien Kabiligi. Wote
wanaendelea kuishi mjini, Arusha, Tanzania,makao makuu ya ICTR katika
nyumba maalum chini ya uangalizi wa mahakama hiyo.
Katika
maombi yaliyotiwa saini na Wakili Philippe Larochelle kutoka Canada,
walalamikaji hao wanataka majaji watoe maombi kwa nchi mbalimbali
kushirikiana ili kuhakikisha kwamba wanapatiwa nchi za kuwapokea kwenda
kuishi kama watu wengine.
Kwa
mujibu wa maombi hayo, Ntagerula anataka kwenda kuishi Canada, Ufaranza
au Uholanzi wakati Kabiligi anapenda kwenda Ufaransa. Kwa upande wao
Bizimungu na Bicamumpaka wanataka kwenda nchini Canada.
Wakirejea
kwenye vifungu vya sheria za ICTR, walalamikaji hao wamekiri kwamba
suala la kutafutiwa nchi za kuishi kwa wanaoachiwa huru na ICTR
halikutajwa kama mojawapo linalozitaka linazozitaka nchi kutoa
ushirikiano pasipo ucheleweshwaji usio wa lazima.
Lakini
wanadai kwamba njia thabiti ya kurekebisha hali hiyo ambayo inakiuka
haki zao za msingi baada ya kuachiwa huru ni kwa mahakama hiyo ya Umoja
wa Mataifa kutumia mamlaka yake ya kisheria kuziomba moja kwa moja nchi
wanamchama wa UN kutoa ushrikiano unaohitajika ili zipatikane nchi za
kuwapokea walalamikaji.
‘’Kuungwa
mkono kwa pendekezo kwamba kupatiwa nchi za kuwapokea ni sahihi unaweza
kupatikana katika maombi lukuki yaliyotolewa na viongozi waandamizi
wote wawili wa mahakama hiyo, Msajili na Rais wake kwenda Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa wakiomba wasaidiwe kutatua tatitizo la
kutopatikana kwa nchi za kuwapokea walioachiwa huru,’’ wanadai katika
sehemu ya maombi yao.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia