MENEJA WA TRA ARUSHA HATARINI KUPELEKWA MAHAKAMANI
MENEJA wa TRA
mkoani Arusha ,Evaristi Kileva yupo
hatiani kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kudharau na kukaidi amri halali ya mahakama iliyotolewa hivi
karibuni ya kutaka akabidhi magari saba ya mshtakiwa Mwale baada ya mahakama kubaini
kwamba hakuna sababu za msingi za kuendelea kuyashikilia.
Mmoja wa wanandugu wa wakili Mwale (jina limehifadhiwa )
alisema kuwa baada ya hukumu kutolewa, mahakama ilitoa order ya kumtaka meneja
wa TRA mkoani Arusha kukabidhi mara moja magari hayo.
Tangu kutolewa kwa
hukumu hiyo, machi 6 mwaka huu meneja huyo amekuwa akipiga danadana kwa
kushirikiana na mawakili wa serikali hatua ambayo inadaiwa huenda ana maslahi
binafsi na magari hayo.
Alisema alipofika katika ofisi za TRA mkoni Arusha na
kuonana na Meneja huyo na kumkabidhi hati ya hukumu pamoja na oda ya mahakama ,chakushangaza
meneja huyo aliendelea kuwasumbua huku
akidai anasubiri majibu kutoka kwa bosi wake makao makuu.
Aliongeza kuwa kwa sasa wapo mbioni kuiomba mahakama
itoe hati ya kumtia mbaroni meneja huyo na kumfungulia mashtaka kwa kosa
la kuvunja sheria za nchi kwa kukaidi amri halali ya mahakama ambayo imekwisha
tolewa .
Awali hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha,Charles
Magesa alitoa hukumu kuwa , wakili Mwale akabidhiwe magari yake baada ya upande
wa serikali kushindwa kuthibitisha uhalali wa kuyashikilia baada ya kudai kuwa
ni matunda ya uhalifu wa kupatikana na fedha chafu.
Mshitakiwa Mwale ambaye kwa sasa bado anashikiliwa
mahabusu katika gereza kuu la kisongo jijini hapa,aliamua kuwasilisha hoja ya
kupinga kukamatwa kwa magari hayo, ambapo kesi hiyo iliunguruma kwa muda huku
upande wa serikali ukiwakilishwa na mawakili ,Fredrick Manyanda na Neema Ringo .
Ambapo mawakili
wa serikai waliiambia mahakama hiyo kuwa, magari hayo yanashikiliwa na mamlaka
ya mapato TRA kwa sababu yalikuwa
hayajalipiwa ushuru wakati yakiingizwa nchini,kitendo ambacho TRA imekuwa ikikanusha
mahakamani hapo na kudai kuwa wao hawadai
ushuru wa magari hayo.
Hakimu Mageza baada ya kupitia hoja za pande zote mbili
alitoa hukumu ya kutaka magari hayo yarejeshwe kwa Mwale ili kupisha kesi ya
msingi iweze kuendelea.
Hata hivyo hukumu hiyo haikuwaridhisha upande wa
serikali na kuamua kukata rufaa mahakama kuu ambapo jaji wa mahakama hivyo
Kakusulo Sambu alipitia hoja za pande zote mbili,kabla ya kutupitia mbali maombi
ya upande wa mashtaka na kubariki hukumu
ya hakimu Magesa ya kutaka magari hayo yarejeshwe kwa Wakili Mwale,
kitendo ambacho hadi sasa kimeshindwa kutekelezwa.
Kwa upande wa Meneja wa TRA Arusha,Evalist Kileva
alipohojiwa kuhusiana na kukaidia amri ya mahakama alisema kuwa kwa sasa hawezi
kulizungumzia suala hilo ila anasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu,bila
kufafanua ni ngazi zipi.
Hata hivyo wanasheria mbalimbali waiwemo wadau wa sheria
hapa nchini wamedai kuwa kitendo cha meneja wa TRA mkoni Arusha,kukaidi amiri
ya mahakama ni kinyume cha sheria na anatakiwa akamatwe na kufunguliwa mashtaka
ya kiidharau mahakama.
habari na mdau wa libeneke la kaskazini Josephy Ngilisho
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia