MKUU WA WILAYA YA HAI APIGA MARUFUKU KILIMO CHA MTONI
mkuu
wa wilaya ya hai bw novatus makunga ametoa mwezi mmoja wa kuondolewa kwa shamba
ya miwa katika chanzo cha mto ngarewarikoi katika kijiji cha mboreni na pia
kuchuliwa hatua za kisheria kwa wamilikiwa wa mifereji wanaopuuzia ratiba ya
kurejesha maji ya mto.
Ameeleza
kuwa hatua hizo zinachukuliwa ili kuokoa
maisha ya wananchi wa maeneo ya vijiji vya tambarare ambao wapo katika hali
mbaya kutokana na hali ya ukame.
mkuu
huyo wa wilaya amefikia hatua hiyo katika kikao alichohitisha cha pamoja kati
ya kamati zinazosimamia matumizi ya maji ya mto huo,viongozi wa vijiji na wataalamu kutoka mamlaka ya bonde la mto
pangani.
Kikao
hicho ambacho pia kilihudhuriwa na madiwani katika kata za mto huo alikihitisha
kwa lengo la kujadili taarifa ya kamati aliyoiunda kufuatilia shughuli za
kibinadamu zinazofanyika katika bonde la mto huo ambazo zinadaiwa kuchangia
upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.
Makunga
alisema kuwa pande zote za watuamiaji wa maji katika mto huo mwamekubaliana
kuondolewa kwa shamba hilo la miwa lililopo katika chemuchemu kijiji cha mboreni
ndani ya mwezi mmoja.
Amesema
baadhi ya ukiukaji wa matumizi ni pamoja na mifereji ya kijiji cha lemira na
nure yam to wawu kutorudisha maji mtoni tangu ilipojengwa na uharibifu wa
korongo la mto kufukiwa na mkulima mmoja.
Kadhalika
amefafanua kamati kugundua chemchem ya kijiji cha mbweera inatakiwa kuoteshwa
miti ya kutuna maji na siyo aina ya mijohoro kwani miti hiyo inakausha maji
pamoja na hatua za kuzuia mifugo kuvamia mto.
Ameeleza
kuwa hatua za haraka ziizofikiwa na kikao hicho ni pamoja na kuhakikisha vijiji
vyote vilivyopo maeneo ya milimani vyenye mifereji kutoka katika mto huo
vinarudisha maji kila ifikapo saa kumi jioni na kuyaancha mpaka asubuhi ya siku
inayofuata
Makunga
alisema kuwa kupitia sheria za mamlaka ya bonde la pangani ambazo ndiyo
zinasimamia matumizi na maendeleo ya mito ya maeneo hayo,watakaobainika
watatozwa faini ya shilingi laki tano
Aidha
amesema kuwa watumiaji hao walikubaliana mifereji yote ikarabatiwe ili
isipoteze maji na pia kuweka milango ya kudhibiti kiasi cha maji na miti ya
asili kupandwa kandokando ya mto na mifereji.
Ameeleza
pia wamekubaliana kusitishwa kwa shughuli za kilimo katika bwawa la magadini
ifikapo mwishoni mwa wezi huu ili liweze kufukuliwa kwa ajili ya kukusanyia
maji na kuyahifadhi
Mmoja
ya mwananchi wa jamii ya wafugaji julius joshua ameeleza kuwa matatizo ya mto
huo yametokana na wataalamu wa kilimo na mifugo kushindwa kuwajibika ipasavyo
Ameeleza
kuwa wengi wamekuwa wakikaa zaidi ofisini bila kufuatilia mto huo ambao uliwahi
kuimarishwa kwa ajili ya kukuza kilimo cha mbogamboga na pia matumizi ya
wafugaji
Naye
mwenyekiti wa kamati ya wananchi hao ya
ufuatiliaji wa korongo la mto huo shaban mahmoudy ameeleza kuwa pendekezo la
kufukuliwa kufukuliwa kwa bwawa la magadini wataliingiza katika mikutano ya
vijiji husika ili liweze kupata Baraka za wananchi wote
Vijiji
vinavotegemea maji yam to huo ni pamoja na msikitini,kambi ya
mkaa,lerai,magadini na kingereka
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia