MAHAKAMA YA BARAZA LA NYUMBA LATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO WA SHAMBA
MAHAKAMA ya baraza la ardhi na nyumba wilayani Arusha
mwishoni mwa wiki iliyopita lililazimika kuendeshea kesi yake nje ya mahakama
hiyo baada ya kutembelea eneo la mgogoro wa shamba lililopo katika kijiji cha Sakila wilayani
Arumeru mkoani Arusha.
Hatua hiyo ilifuatia baada ya shauri nambari 35 la mwaka
2005 lililofunguliwa mahakamani hapo na mdai,Augustino Nko dhidi ya kanisa la
International Evangalisim Church ambapo anadaia kuporwa ardhi na kanisa hilo
kwa kuingilia mipaka ya shamba lake.
Hatahivyo,malumbano makali yaliibuka wakati wa kufika katika
eneo la tukio ambapo ilimlazimu mwenyekiti wa baraza hilo,Dorith Mangure
kuamuru eneo lenye mgogoro lipimwe ukubwa wake sanjari na mipaka yote ili
kuondoa utata.
Akizungumza kabla ya zoezi la kukagua na kupima mipaka ya
eneo hilo,Mangure alisema kwamba lengo
kuu la baraza lao kufika kijijini hapo ilikuwa ni kupima ukubwa wa eneo hilo
sanjari na mipaka yote iliyopo katika eneo hilo ili kujiridhisha zaidi.
Hali hiyo iliwalazimu baadhi ya watumishi wa baraza hilo
kumwapisha kwa kiapo shahidi kutoka upande
wa washtakiwa,Ndewario Isangywa kwa lengo
la kuonnyesha ukubwa na mipaka ya eneo hilo baada ya shahidi wa
kwanza,Elisa Nko kukataliwa na upande wa walalamikaji.
Mara baada ya kukamilsha zoezi la upimaji huo,Mangure alisema kwamba eneo
hilo lina ukubwa wa ekari 2.3 ambapo upande wa kusini linapakana na familia ya
Robert Meshack,upande wa kazkazini linapakana na chuo cha bibilia cha kanisa la
IEC,upande wa mashariki linapakana na familia ya Winston Nko na upande wa magharibi
linapakana na familia ya marehemu mzee Meshack Nko.
Mara baada ya kufafanua vipimo hivyo alisema kwamba baraza
lao limekusanya ushahidi mbalimbali ambapo uitawasilishwa kwa jaji wa mahakama
hiyo kwa lengo la kupanga tarehe ya kutoa uamuzi kuhusiana na sakata hilo.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo wakili upande wa walalamikaji ,Duncan Oola alisema kwamba mteja
wake alifungua kesi mbele ya baraza hilo kulalamikia kitendo cha kanisa hilo
kuingilia eneo lake na ndio sababu iliyopelekea baraza hilo kutembelea eneo
hilo.
Oola,alisema kwamba mteja wake alifungua kesi mbele ya baraza hilo mwaka 2005 na kisha
kushindwa mwaka 2007 hatahivyo alikata rufaa mwaka huo huo kwa kile alichodai
ya kwamba hakuridhika na uamuzi wa baraza hilo.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia