LUBANGA JELA MIAKA 14, MAHAKAMA UFARANSA YAZUIA MNYARWANDA KUREJESHWA KWAO
Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, wiki hii imemhukumu
kifungo cha miaka 14 jela kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga, kwa uhalifu wa kivita,
Mahakama ya juu nchini Ufaransa imebatilisha uamuzi wa kumrejesha raia
wa Rwanda kwao ili akashitakiwe kwa makosa ya mauaji ya kimbari.
ICC
Lubanga apata miaka 14 jela: Majaji wa mahakama hiyo
Jumanne wiki hii walimhukumu kifungo cha miaka 14 jela kiongozi wa
waasi katika DRC, Thomas Lubanga, kwa uhalifu wa kivita. Hukumu hiyo
imepokelewa vema, huku serikali ya DRC ikisema ni ishara chanya kwa
amani ya baadaye katika jimbo lenye migogoro la Kivu. Wakati muungano wa
Mahakama ya Kimaifa ya Makosa ya Jinai ukielezea uamuzi huo kama tukio
muhimu katika kupambana na uonevu katika jimbo hilo, upande wa mashitaka
umesema umepeleka ujumbe ulio wazi kwamba wahusika wa makosa hayo
hawataachwa bila kuadhibiwa.
Wakili wa waasi wa Darfur aomba msaada UN:
Jumatano wiki hii wakili wa Abdallah Banda na Mohammed Jerbo aliliomba
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuichulia hatua serikali ya Sudan
kwa madai ya kuzuia haki isitendeke kwenye kesi ya wateja wake. Karim
Khan alielezea kuwa upande wa utetezi hauwezi kufanya uchunguzi wa
maaana kwa sababu Sudan imekataa kushirikiana na mahakama. Washitakiwa
wote wanatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia
shambulizi la 2007 katika ngome ya kijeshi ya Haskanita, ambapo walinda
amani wa kimataifa 12 waliuawa.
Kesi ya Wakenya wanne kuanza Aprili 2013:
Mahakama Jumatatu wiki hii ilipanga Aprili 10 na 11, 2013, kama tarehe
za kuanza kwa kesi mbili za Wakenya wanne, ambao ni Naibu Waziri Mkuu
Uhuru Kenyatta, Mbunge William Ruto, aliyekuwa Mkuu wa Utumishi, Francis
Muthaura na Mwandishi Joshua arap Sang. Wanatuhumiwa kwa makosa ya
uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi
mkuu wa rais mwaka 2007.
UFARANSA
Mahakama yazuia raia wa Rwanda kurejeshwa kwao:
Mahakama ya Juu nchini Ufaransa imebatilisha maamuzi ya awali
yaliyotolewa Machi 29, na Mahakama yaRouen kwamba Claude Muhayimana
anapaswa kurejeshwaRwanda kukabiliana na makosa ya mauaji ya
kimbari.Rwanda inamhitaji Muhayimana kwa makosa yaliyotendeka katika
mkoa wa Kibuye mwaka 1994.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia