WANANCHI WATEMBEA UMBALI MREFU KUFATA MAJI KUOFIA KIVUKO
Kivuko cha sasa cha gogo la mti
mkuu wa wilaya akiwa anajitaidi kushuka katika korongo
Diwani
wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa akitoa maelezo kwa mkuu wa
wilaya ya hai Novatus Makunga kuhusu kivuko cha Mande ambacho kimezolewa
na mafuriko ya mvua katika mto weruweru Mwezi Januari mwaka jana
Wananchi
wa vijiji vitano katika kata ya Machame Mashariki wilayani Hai kwa zaidi ya
mwaka sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma mbalimbali kwa
kuogopa kutumia kivuko cha gogo la mti katika eneo la Mande katika Mto Weruweru.
Uoga
huo unatokana na kufariki dunia kwa mama na binti yake walioteleza na kusombwa
na maji katika mto Weruweru
wananchi
wa vijiji vya nkuundoo na nkuusinde vilivyoko machame mashariki wamemueleza
mkuu wa wilaya ya hai bw novatus makunga kwamba eneo hilo la mande lilikuwa na
kivuko ambacho kilisombwa na maji kufuatia mafuriko ya mto weruweru mapema
mwaka jana
Hamiliton
swai,mkazi wa kijiji cha Nkuusinde ameeleza kuwa baada ya kuteleza na kusombwa
kwa mama huyo akijaribu kumuokoa binti wananchi wa vijiji hivyo wanalazimika
kuzunguka kupitia daraja lililopo karibu na nyumba ya Mengi
Akifafanua
kuhusu kifo cha huyo mama,Swai alisema kuwa baada ya kuteleza kwa binti yake
naye alijaribu kumfuata kwa lengo la kumuoko ndipo waliosombwa na maji na
baadaye miili yao kukutwa wakiwa wameshafariki dunia.
Anasema
kuwa walikuwa wanatoka kukoboa mahindi katika mashinne zilizoko upande wa pili
wa mto huo mkubwa.
Diwani
wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa alisema kuwa huduma ambazo zipo kila
upandew haziwezi kuepukika na wananchi na hivyo kusababisha maingiliona ya mara
kwa mara
Alisema
kuwa kivuko cha mande ni muhimu kutokana na kutumiwa na jamii za pande hizo
wakiwemo wanafunzi,waumini wa dini na wagonjwa
Alitaja
huduma za kijamii ambazo wananchi wanalazimika kuzifuata kwa kila upande wa mto huo kuwa ni pamoja na kanisa la Lyamungo Umburi
na kituo cha afya cha Umburi pamoja na shule za sekondari Lyasiska,Lyamungo na Nkuu
Huduma
nyingine ni zahanati ya Nkweshoo pamoja na mashine ya kukoboa nafaka na kukamua
mafuta ya alizeti zilizoko katika chama
cha ushirika cha machame nkuu nkuu
Akizungumza
mara baada ya kukagua eneo hilo mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza
kutokana na umuhimu wa kivuko hicho cha mande kwa jamii tayari gharama za
kukirejesha kiasi cha shilingi milioni 62.1 zimewekwa katika bajeti ya usafirishaji
wa serikali la mitaa(LGTP)
Makunga
alisema kuwa kutokana na kivuko hicho kutegemewa na idadi kubwa ya
wananchi,serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa tatizo hilo la kivuko cha
awali kusombwa na maji ya mafuriko katika mto Weruweru




0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia