SEREKALI KUTHAMINI MAFUNZO YA UFUNDI STADI
Serekali imesema inathamini mafunzo ya ufundi
stadi na sanifu hapa nchini kutokana na umuhimu wake katika kuendesha
viwanda ,ujenzi na kilimo na kuwa mafundi hao ni muhimili mkuu wa
kuongeza thamani ya rasilimali zetu.
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa elimu na mafuzo ya ufundi Philipo Mulugo kwa hotuba iliyosomwa na mkurugenzi wa elimu na mafuzo ya ufundi David Kavuza kwenye mahafali ya mafunzo unganishi na kozi ya awali kwenye chuo cha ufundi Arusha jana na kuwataka vijana wanaomaliza veta kutodhani kuwa hapo ndiyo mwisho badala yake kujiunga na kozi za ufundi kwa ngazi ya diploma kwenye chuo hicho.
Mulugo alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kozi hii (BRIDGING COURSE) kufanyika hapa nchini na pia kozi ya awali yenye madhumuni ya kuwajengea uwezo vijana na kuwapa sifa zinazohitajika kujiunga na mafunzo mbali mbali ya ngazi ya ufundi sanifu yanayotolewa na vyuo vya ufundi hapa nchini kikiwemo chuo cha ufundi Arusha.
Kwa hili wizara ya elimu ililiratibu kwa kuandaa mitaala ya kozi unganishi ili kuwawezesha wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi(VETA)kujiunga na mafunzo ya ufundi sanifu(National Technical Awads)na kusimamiwa na (NACTE) kwa majaribio na mitaalailiandaliwa katika fani za umeme na mitambo pamoja na masomo shirikishi ya hisabati na fizikia na lugha(communication skills) nayo yalihusishwa na pia iliandaliwa na wadau mbali mbali kutoka vuo vya ufundi stadi na ufundi sanifu na kufanyiwa majaribio mwaka wa 2011-12.
"bahati mbaya chuo pekee kilicho endesha kozi hii ni Arusha kwani tulitoa wito kwa vyuo vyote vya ufundi kuanzisha kozi hii lakini imekuwa kinyume na maagizo yetu na kupongeza mkuu wa chuo kwa hili"alisema mulugo.
Nae kaimu mwenyekiti wa chuo hicho Suzan Mnafe mafunzo hayo yanapanua wigo wa elimu ya ufundi na pia yanafungua milango kwa wahitimu wa mipango ya veta kujiendeleza kulingana na uwezo wao wa kitaaluma na kuwa chuo kupitia mafuzo hayo kimeongeza udahili wa wasichana kwa mwaka kutoka wanafunzi 40 kwa mwaka 2008-9 hadi kufikia wanafunzi 123 ambayo ni 30% katika mwaka ujao wa masomo2012-13.
Mnafe alisema kuwa pamoja na udahili kwa watoto wa kike kuongezeka bado chuo kinakabiliwa na ukosefu wa malazi kwa watoto hao kwani kati ya watakaodahiliwa123 ni watoto16 ndo watakaopata malazi chuoni hapo wengine 107 itabidi wajitegemee hali inayohatarisha ushiriki wao kikamilifu katika mafuzo yao.
Nae mkuu wa chuo hicho dkt.Richard Masika alisema kuwa majukumu ya chu hichi ni kutoa mafunzo ya ufundi na sayansi katika fani mbali mbali za uhandisi,sayansi na teknolojia pia kufanya utafiti matumizi (Applied Research) na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa jamii(consultancy) na pia chuo baada ya kupata ithibati na kuanzisha mafunzo haya kilipata ithibati ya kutoa na kuanzisha mpango wa kutoa digrii katika nyanja za uhandisi,ujenzi na umwagiliaji hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika mipango ya taifa ya mkukuta,kilimo kwanza nampango wa taifa wa maendeleo wa 20101-25..
Masika alisema kuwa mpango huu unaondoa kilio cha muda mrefu kutoka kwa wadau mbali mbali kuwa elimu ya veta sio endelevu na pia yataondoa dhana potofu kuwa mafuzo ya Veta ni kwa ajili ya wenye ufaulu dhaifu na wasioweza kujiendeleza na taifa litapata watu watakaozitumia rasilimali zetu vizuri.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia